Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MAWAZIRI WA SERIKALI YA WAMU YA TANO WATAPISHANA KWA MASAA MKOANI KAGERA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kagera kuanzia tarehe 14-16 ...




Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kagera kuanzia tarehe 14-16 Julai, 2016.
Siku ya kwanza ya tarehe 14 Julai, 2016  Mwakyembe anatarajia kukutana na kuongea  na wadau waliopo chini ya Wizara yake ya Sheria na Katiba pamoja na Vyombo vya Habari katika Ukumbimbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuanzia saa 6:00 hadi saa 7:00 Mchana. Aidha kuanzia saa 7:30 hadi 8:30 mchana atatembelea ofisi za RITA kujionea uandikishaji wa watoto waliochini ya miaka mitano.

Katika siku ya pili ya tarehe 15 Julai, 2016 Mwakyembe atatembelea Gereza la Wafungwa la Mkoa wa Kagera, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Manispaa ya Bukoba ili kuongea na uongozi wa ofisi hizo ambazo zipo chini ya Wizara yake.

Siku ya tatu ya tarehe 16 Julai, 2016 Mwakyembe akiwa mkoani Kagera ataelekea Wilayani Biharamulo ambapo atatembelea Gereza la Wafungwa Biharamulo na kuhitimisha ziara yake katika Mkoa wa Kagera na kuondoka kuelekea Mkoani Mwanza.



WAKATI   HUO  HUO  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto Ummy Mwalim anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera kuanzia tarehe 15-16 Julai, 2016.

Katika ziara hiyo Ummy Mwalim anatarajia kuzindua wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana siku ya Ijumaa tarehe 15 Julai, 2016. Mara baada ya uzinduzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Waziri ataelekea Wilayani Muleba kutembelea Hospitali Teule ya Wilaya ya Rubya.

Katika siku yake ya pili Mkaoni Kagera tarehe 16 Julai, 2016 Ummy Mwalim atatembelea kituo cha kuwatunza wazee Kiilima kilichopo Wilyani Bukoba kuanzia saa 4:00 asubuhi. Kituo hicho cha Kiilima kipo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto ambapo kwasasa kinawatunza wazee 18 wanaume wakiwa 14 na wanawake 4 pamoja na watoto yatima10.

Wito kwa wananchi wote hususani wanawake wanaombwa kuhudhuria kwa wingi hasa kwenye uzinduzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kushuhudia Waziri akizindua wodi ya wazazi ambapo mara baada ya uzinduzi wa wodi hiyo huduma kwa wazazi zitaimarika zaidi na kupunguza msongamano kwa kiasi kikubwa katika wodi ya wazazi ya zamani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top