Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MISS BARABA GIRLS SECONDARY SCHOOL
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
  Wanafunzi   wametakiwa   kushiriki   michezo   mbalimbali   wanapokuwa   shuleni   kwani   kufanya   hivyo   kunawasaidia   ...




 Wanafunzi  wametakiwa  kushiriki  michezo  mbalimbali  wanapokuwa  shuleni  kwani  kufanya  hivyo  kunawasaidia  wao  kuwa  na  wigo  mpana  wa  kujiajiri  nje  na  kutegemea  elimu  ya  darasani   tu.

 
Wito  huo  umetolewa  na  Miss  Baramba  Sekondari  kwa  mwaka  2016 Jovither Dominick  wakati  akiongea  na  Redio  Fadeco  mara  baada  ya  kutangazwa  mshindi  wa  taji  hilo  kwa  mwaka  huu katika  tamasha  la  utamaduni  shuleni  hapo  ambalo  hufanyika  kila  mwaka  na  kuhusisha  michezo  mbalimbali  ya  kitamaduni.






Amesema  kuwa  kupitia  michezo  fani  mbalimbali  ambazo  zimejificha  kwa  wanafunzi  ni  nyingi  hivyo  zinahitajika  kuwa  tayari  kushiriki  pale  wanapopata  fursa  ya  kuelekezwa  au  kuhimizwa  na  walimu  wao.

Jovither  Dominick  amesema  yeye  kuwa  Miss  Baramba  Sekondari  inawezekana  ikwa  mwanzo  wa  kufungua  milango  ya  kujihusisha na  fani  hiyo  huku  akisema  kuwa anaweza  kujiongezea  kipato  kwa  kutoa  ushauri  hata  kama  atakuwa  ameajiriwa  kwa  fani  nyingine  tafauti  na  urembo






 Zawadi  kwa  Miss  Baramba  alijipatia  Cherehani,Mshindi  wa  Pili  akijipatia  HIACE  COOKER,watatu  Redio  ya  Sub UFA, na  washindi  wa Anna  Makinda  House wakijipatia  laki  saba  taslimu,mshindi  wa  pili  laki  tatu na Mshindi  wa  tatu  laki  moja  na  nusu.

 Katika  siku  hiyo  ya  siku  ya  utamaduni  maarufu  kama  CULTURAL  DAY  kulekuwepo  na  mashindano  ya  kumpata  mshindi  wa  jumla  ambao walikuwa  wakishindana  kwenye  vipengele  vya ngoma, kuimba,  maingizo  ambao  makundi  yalikuwa  matatu  ambayo  yamepewa   majina  ya  Ana  Tibaijuka,Ana  Makinda  na  Asha  rose  Migiro  hiyo  hutumika  kutambulisha  wanawake  walioonyesha  mfano  wa  kuongoza.

 Mshindi  wa  jumla  mwaka  2016  ni  Ana  Makinda  House, Asha  rose  Migiro  House  ikishika  nafasi  ya  pili  na  Ana Tibaijuka  ikashika  nafasi  ya  tatu  ikiwa  imeangushwa  na  baada  ya  kutangazwa  washindi  walikuwa  na  haya  ya  kusema.




Kwa upande  wao  washiriki  wa  shindano  hilo  la  miss Baramba  Sekondari  mwaka 2016  wameelezea  kuridhika  na  majaji  wa  shindano  hilo  kuwa  wameonesha  haki  na  wakasema  wanajivunia  hatua  waliofikia  huku  wengine  wakieleza  furaha  yao.











About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top