Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: VIONGOZI WA DINI WILAYA YA KARAGWE MKOANI KAGERA WATAKA AMANI ITUNZWE
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Kamati   ya   Amani   na   Maadili   ya   wilaya   ya   Karagwe   mkoani   Kagera   inayoundwa   na   viongozi   wa   dini   kuto...




Kamati  ya  Amani  na  Maadili  ya  wilaya  ya  Karagwe  mkoani  Kagera  inayoundwa  na  viongozi  wa  dini  kutoka  madhebu  mbalimbali  ya  kikristo  na  uislamu   imewataka  wananchi wa  wilaya  ya  Karagwe  kutunza  na  kudumisha  amani  iliyopo  ili isipotee  kwani  ikipotea  kuirudisha  siyo  rahisi.


Wametoa  kauli  hiyo  katika  kikao  chao  cha  pamoja  na  mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe  Godfrey  Mheluka  kilichofanyika  kwenye  ukumbi  wa  ofisi  ya  mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe.


Viongozi  hao  wamesema  amani  iliyopo  inabidi  kutunzwa  kwa  gharama  yoyote  ile  kwani ikipotea  kuirudisha  siyo  rahisi  kama  ambavyo   baadhi  ya  watu  wanataka  kuichezea  amani  iliyopo  hivyo  wakawataka  wananchi  pamoja na  waumini  wao.

Askofu  wa  jimbo  Katoliki  la  Kayanga  Almachius  Vicent  Rweyongeza  ambaye  ni  mlezi  wa  kamati  hiyo  ya  Amani  na  Maadili  amesema  wao  viongozi  wa  kiroho  wanazo  kazi  tatu  kwenye  wito  waliokubali  kuutumikia  ambapo  anabainisha  hapa.



Amesema  katika  kutumikia  Mungu  awategemei  malipo  lakini  Mungu  mwenyewe  huwalipa  kazi  hiyo  kwa  kuwapatia  afya  njema  hivyo  kumtambua  ni  muhimu  na amesema  maandamano  yoyote  hayawezi  kuleta  tija  kama  mtu  au  watu  hawataweza  kufanya  kazi  kwa pamoja.



Katibu wa  kamati  ya  Amani  na  Maadili  Mdashiru   Kalokora  ambaye  pia  ni  katibu  wa  Baraza  la  Waislamu  Tanzania   BAKWATA  wilaya  ya  Karagwe  na  Kyerwa  amesema  kamati  hiyo  imekamilika  na  imezingatia uwiano  sawa  hivyo  akawataka  wananchi  kuipa  ushirikiano.



Makamu  mwenyekiti  wa   Kamati  hiyo  ya  Amani  na  Maadili  naye  pia  ameweza  kusema  kuwa  utii  wa  mamlaka  kwa  kufuata  misingi  iliyowekwa  itasaidia  kudumisha  amani  na  kuongeza  kuwa kitu  kikiwepo  watu  hawaezi  kuona  umuhimu  wake  lakini  kikiondoka  ndiyo  hutambua  hilo  hivyo  akawasihi  wananchi kutothubutu  kuipoteza Amani.

Hata  hivyo  Mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe  amewahakikishia  wajumbe  wa  kamati  hiyo  kuwa  watakuwa  ni  sehemu  ya  kamati  ya  ulinzi  na  usalama  ya  wilaya  na  kuongeza  kuwa  watakayojadili  na  kufikia  uamuzi  watayaheshimu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top