Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KUNDI LA WHATSAPP LA MAAFISA USTAWI WA JAMII TANZANIA LAONYESHA MFANO WA KUIGWA KWA KUTOA MSAADA KAGERA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Na:   Sylvester Raphael Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania waliosoma Shahada ya Sosholojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka ...

Na:  Sylvester Raphael

Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania waliosoma Shahada ya Sosholojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 2001 na kuhitimu Mwaka 2004 wameonyesha mfano wa kuigwa na wahitimu wa kada mbalimbali kwa umoja wao ambao umetoa mifuko tisini ya saruji kusaidia waathirka wa tetemeko mkoani Kagera.





Akitoa msaada huo Kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum M. Kijuu kwa niaba ya wenzake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kagera Bi Rebbeca Gwambassa alisema kuwa  walihitimu Shahada ya Sosholojia chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2004 na wana kundi la mtandao wa kijamii la WHATSAPP ambalo limeguswa na janga lililotokea mkoani Kagera na kuamua kuchangia.


Bi Rebbecca alisema kundi lao lina Maafisa Ustawi wa Jamii 100 na walichangishana na kufikisha kiasi cha shilingi 1,520,000/= ambazo waliamua kununua Saruji mifuko 90 na kuikabidha kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera ili iwasaidie waathirika wa tetemeko kwa kurudisha miundombinu iliyoharibiwa.


Aidha, Bi Rebbecca alisema kuwa wao kama wataalamu wa masuala ya kijamii wameamua kutoa msaada huo kwa  kuonyesha mfano kwa wanataaluma wengine kuwa mitandao ya kijamii inatakiwa kutumika kwa kuleta mabadiliko kwenye jamii na siyo kuitumia mitandao hiyo kwa mambao ambayo hayana faida katika jamii.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu akipokea msaada huo aliwashukuru wanataaluma hao na kwakuonyesha mfano hasa kupitia katika umoja wao wa kundi la Whatsapp kwa kuchangishana na kutoa msaada wa mifuko 90 ya saruji kwa ajili ya kuwasaidia Wanakagera .




“Kama kila kundi la Whatsapp hapa nchini likiamua kuchangia kidogo kidogo hata mifuko kumi tu ya saruji wananchi wa Kagera watakuwa wamepata msaada wa kutosha. Ninatoa wito kwa wanataaluma wengine kupia makundi yao mbalimbali ya mitandao ya kijamii kujitoa kama kundi la Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania walivyoonyesha mfano katika kuchangia maafa Kagera .” Alisistiza Mhe. Kijuu.


Hadi sasa mkoa wa Kagera umepokea misaada ya mahitaji mbalimbali yenye thamani ya shilingi 1,700,000,0000/=  ambapo tayaria miundombinu mbalimbali kama shule, zahanati, vituo vya afya na barabara  imeanza kujengwa ili wananchi warejeshewe huduma za kijamii.



Katika hatua nyingine Tume ya ushindani Tanzania imetoa msaada wa msaada wa mabati 5,743 sawa na bandari 360 yenye thamani ya shilingi 86,145, 000/=. Pia na shirika la KADERES la wilayani Karagwe kupitia shirika la Direct Relief la nchini Marekani wametoa madawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya 40,000,000/=

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top