Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WITO KWA WATANZANIA KWA VIONGOZI NA WANANCHI KWA UJUMLA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi wilayani Karagwe mkoani Kagera wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika harakati zake za kupambana i...

Wananchi wilayani Karagwe mkoani Kagera wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika harakati zake za kupambana ili kuleta maendeleo katika taifa la Tanzania akioonesha kufuata nyayo za Baba wa Taifa hayati Mwalim Julius Kambarage Nyerere.

Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumzia kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa ambayo hufanyika kila oktoba 14 kila mwaka.

Wamesema kuwa  Hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere anakumbukwa kwa mambo mengi ikiwemo kutetea wanyonge,kukataa ukabila, udini, Rushwa pamoja na vitendo vya unyanyasaji ambavyo katika uongozi wa awamu zilizopita vilikuwa vimeshamili na kuifanya nchi ya Tanzania kuonekana ya wachache lakini kwa uongozi huu wa Rais Magufuli unatia matumaini kwa walio wengi.

Aidha wameasa wananchi wenzao kufanya kazi kwa bidii ikiwa ndiyo njia mojawapo ya kuendelea kumkumbuka baba wa Taifa kwani alikuwa mchapakazi na mzalendo kwa taifa lake huku wakiowaomba viongozi wote wa serikai kufuata nyayo hizo ili kuliweka taifa la Tanzania katika hali ya amani,utulivu ,haki na usawa.

Hata hivyo wananchi walioongea na kituo hiki wameeleza kuwa na matumaini na uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli wakisema kuwa kufikia 2020 atakuwa amerudisha nchi kama ilivyokuwa wakati wa uongozi wa hayati Mwalimu Nyerere.

Itakumbukwa kuwa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki dunia  mnamo tarehe 14 mwezi wa 10 mwaka 1999 ikiwa ni kumbuka ya miaka 17 tangu kifo chake.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top