Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KIJIJI CHA KASHANDA KUNUFAIKA NA UJENZI WA ZAHANATI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Shilingi milioni 300 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa   zahanati ya kijiji cha Kashanda katika kata ya Kabilizi wilayani Muleba il...

Shilingi milioni 300 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa  zahanati ya kijiji cha Kashanda katika kata ya Kabilizi wilayani Muleba ili kupunguza hadha inayowakabili wananchi wa kijiji hicho.

Diwani wa Kata ya Kabilizi  Salmoni Karugaba amesema kuwa fedha hizo zimeshapitishwa na baraza la madiwani  katika bajeti ya mwaka 2017/2018 kwa ajili ya ujenzi huo .

Amesema kuwa  wakati wakisubiri fedha hizo kutoka serikalini wananchi wameshaanza kujitolea mawe, mchanga na matofari kutokana na hadha kubwa wanayoipata ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa kumi kufata huduma ya afya.

Amesema kuwa kata hiyo yenye vijiji vinne ina zahanati moja tu iliyoko katika kijiji cha Kiwela hali iliyopelekea   wananchi wa vijiji vingine kutembea umbali mrefu kufata huduma ya afya .

Aidha amesema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo ukikamilika utaweza kuhudumia wananchi wengi wa kata hiyo ambapo wanatarajia kuanza ujenzi huo   mwishoni mwa mwezi January mwaka huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top