Home
»
»Unlabelled
» JIBU HILI SIJUI Laendelea Kutawala Ufisadi Wa Mabilioni NIDA....Yadaiwa Kitambulisho Kimoja Kimegharimu Sh 89,800
Wingu
zito limetanda ndani ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhusu
matumizi ya Sh bilioni 179.6 ambako kila kitambulisho cha taifa
kimegharimu Sh 89,800 zikiwamo gharama za utawala
Hayo
yamebainika siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kushangazwa na
watendaji wa mamlaka hiyo ikizingatiwa vitambulisho vilivyokwisha
kutengenezwa hadi sasa havifiki milioni mbili na havina saini.
“Utaona
ugumu wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina. Wapo watu
wanacheza na fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana wengine
wanataka bodi zao wakakae Ulaya.
“Hapo
ndipo tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara wa Sh milioni 35 kwa
mwezi…naomba mniombee kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa
hawa wanaotaka kuifikisha nchi pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.
Rais
Dk. Magufuli, licha ya kushangazwa na hali hiyo, alisema Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) ilipewa Sh bilioni 70 lakini iliweza kutengeneza
vitambulisho 23,253,982 ambavyo vilikuwa na saini ya kila mpiga kura
na kila kimoja kimegharimu Sh 3,010.
Kutokana na hali hiyo, tofauti ya gharama kati ya kitambulisho kimoja cha NIDA na cha NEC ni Sh 86,790.
Pamoja
na hayo, hivi sasa Watanzania wanasuburi ripoti ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad, kuhusu
matumizi ya fedha hizo za NIDA.
Januari
26 mwaka huu, Rais Magufuli alitangaza kumsimamisha kazi ili kupisha
uchunguzi dhidi yake, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu.
Maimu alisimamishwa kazi pamoja na maofisa wengine wanne, kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Serikali.
Maofisa
hao ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Joseph
Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina
Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.
Akitangaza
uamuzi huo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alisema taarifa
zilizomfikia Rais zinaonyesha kuwa NIDA hadi wakati huo ilikuwa imetumia
Sh bilioni 179.6, kiasi ambacho ni kikubwa.
Alisema
Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi kujua jinsi fedha hizo
zilivyotumika, maana amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana
na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.
Licha
ya kumuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, afanye
ukaguzi maalumu wa hesabu za NIDA ukiwamo ukaguzi wa “value for money”
baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi
sasa, pia aliitaka Takukuru ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa
na vitendo vya rushwa au la.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Recent Posts
- ADC Summit 2025!09 Jan 20250
The African Disability Collaboration (ADC) is thrilled to host the ADC Summit 2025 under the ...Read more »
- KAGERA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KUENDELEA KUJIIMARISHA KUWALINDA RAIA NA MALI ZAO25 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Vyombo ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya ...Read more »
- MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA WILAYA ZA KARAGWE NA NGARA PIA HITIMISHO WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mwenge wa Uhuru waendelea kuchanja mbuga Mkoani Kagera kwa ku...Read more »
- MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI KAGERA NA KUANZA UZINDUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YABILIONI 1216 Apr 20180
Na: Sylvester Rapahel Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na...Read more »
- TIMU YA WATAALAM WA UJENZI KUTOKA NCHINI CHINA YAKAGUA ENEO LA UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA ILI KUANZA UJENZI MARA MOJA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Serikali ya Watu wa China yatuma timu ya Wataalam wa Usanif...Read more »
- MKOA WA KAGERA WAVUKA LENGO KATIKA UNDIKISHAJI WA WANAFUNZI AWALI NA DARASA LA KWANZA MWAKA 201816 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mkoa wa Kagera wavuka lengo la uandikishaji wa Wananfunzi katika madarasa...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.