Mkuuu wilaya ya Karagwe Deodatus Kinawiro ametatua
mgogoro wa ardhi wa wanakijiji cha
Omkakajinja na wamiliki wa block no5 na
6 kwa kueleza kuwa block hizo ziko ndani
ya kijiji hicho na sio nje kama ilivyokuwa inafahamika hapo awali.
Akiongea na wananchi wa kijiji cha Omkakajinja
Kinawiro amesema kuwa block namba 05 na 6 ambazo zilikuwa zinaleta mgogoro kwa
wananchi wa kijiji hicho wakidai kuwa block hizo ziko nje ya kijiji ameeleza
kuwa madai hayo sio sahihi na badala yake watambue kuwa block hizo ziko ndani
ya kijiji cha Omkakajinja na mmiliki wa block anabaki kuwa mwekezaji tu.
Ameeleza kuwa block zimewekwa kwa mjibu wa sheria
hivyo zinatakiwa kutumika kwa ajili ya kufugia na sio kufanyia shughili
nyingine.
Wakati mkuuu wa wilaya akitoa maelezo hayo wananchi
wameeleza kutoridhika wakitaka ardhi irudi mikononi mwao na sio kubaki katika
mikono wa wamiliki wa ardhi kwani tangu wafukuzwe katika ardhi hiyo mwaka 1970
wanaishi kwa kutanga tanga na hawana sehemu ya kulima au kufanya shughuli
nyingine za maendeleo.
Hata hivyo mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha
Omkakajinja amesema kuwa wako tayari kufikisha suala hili mahakamani ili kupata
haki ya kumili ardhi yao huku akieeleza kutiokubaliana na maamuzi ya mkuu wa
wilaya.
Post a Comment