Wananchi wilayani Karagwe mkoani Kagera wamepewa
tahadhari ya uharibifu wa mazingira huku wakitakiwa kutoa taarifa katika
uongozi husika pale watakapokuta mtu yoyote akijihusisha na vitendo vya
uharibifu wa mazingira.
Tahadhari hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya
Karagwe Deodatus Kinawiro kufuatia kukamatwa kwa baadhi ya watu wanaojihusisha
na vitendo vya ulimaji wa bangi katika kata ya Rugera wilayani humu.
Kinawiro amesema kuwa ulimaji wa bangi ni marufuku
katika nchi ya Tanzania kwani ni mojawapo ya uharibifu wa mazingira na bangi ni
hatari kwa afya hususani kwa vijana ambao wanashiriki katika uvutaji wa bangi
huku akieleza kuwa atakayekamatwa anafanya hivyo atachukuliwa hatua za
kisheria.
Hata hivyo amesema kuwa kamati ya ulinzi na Usalama
wilaya ya Karagwe kwa kushirikiana na Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera
wameanzisha operasion ya kukagua watu wote wanaolima bangi na itakuwa endelevu
hivyo kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha zoezi
hilo.
Amekemea watu wanaokata miti ovyo
kwa ajili ya mkaa au matumizio mengine na wale wanaolima katika vyanzo vya maji
akisema kuwa hao wakitamatwa pia watachukuliwa hatua za kisheria
Post a Comment