Uongozi
wa hospital ya rufaa ya Missenyi Mugana hospitali umeiomba serikali kupanua wodi
ya akina mama wajawazito ili kupunguza msongamano ulioko pale hosipitalini.
Akizungumza
na waandishi wa habari katibu wa hosipitali hiyo sisita
IMVIOLATA TEMBA amesema wodi ya akina mama wajawazito inavitanda 24 ambapo watu
wanaokuja kujifungua ufikia 40 hadi 60 khali inayopelekea wanawake hao kulala
chini.
TEMBA
amesema kuwa mpaka sasa hosipitali hiyo inahudumia wagonjwa wengi kutoka nje ya
wilaya hiyo hivyo inahitaji kufatiliwa kwa ukaribu ili kuboresha huduma za
afya.
Aidha
amezungumzia suala la bajeti inayotengwa na hosipital hiyo ambapo amesema kuwa
kila mwezi hutumia zaidi ya milion 50 ikiwa bajeti inayotengwa na serikali ni
milioni 75 kwa mwaka.
Post a Comment