Mkuu wa wilaya ya Karagwe
Deodatus Kinawiro ametekeleza agizo la Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muuungano wa
Tanzania alilolitoa hivi karibuni la kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi
wa kijiji cha Kishoju na Dayosisi ya Karagwe mgogoro ambao ulianza tangu mwaka 1980 ukihusisha
hekta 422 zilizochukuliwa na Dayosisi.
Akiongea wananchi wa kijiji
cha Kishoju leo Kinawiro amesema kuwa yeye ni kiongozi ambaye anatumikia
wananchi wote kwa kufuata misingi ya sheria ,kanuni na taratibu za nchi ambapo
amewaeleza wananchi kuwa wakati wa kugawa ardhi hiyo kwa Dayosisi ya Karagwe
utaratibu wote ulifuatwa na hadi kuwapatia hati miliki hivyo hadi sasa
inafahamika kuwa ardhi hiyo ni mali ya Dayosisi na wananchi wote ambao wako
katika maeneo hayo wanatakiwa kutoka ili shughuli za Dayosisi ziweze kuendelea
kwani ni kwa ajili ya maeneleo ya Wanakaragwe wote.
Kinawiro amesema kuwa ifikie
wakati sasa wananchi waachane na migogoro isiyokuwa ya lazima na badala yake
wajikite katika shughuli za maendeleo ambazo ziko mbele yao,kwani migogoro
ambayo wanaiendekeza haitakuwa na msaada kwao katika maisha ya baadae.
Hata hivyo maamuzi ya mkuu
wa wilaya hayakuwaridhisha wananchi wengi na viongozi wa serikali ya kijiji
hicho huku wakieleza kuwa kwa sasa wakitolewa katika maeneo hayo ambayo
wanafanyia shughuli zao za kilimo hawatakuwa na sehemu nyingine ya kwenda japo
malalamiko hayo yametupiliwa mbali na mkuu wa wilaya akieleza kuwa hakuna anayetakiwa
kuendele kufanya shughuli katika ardhi hiyo isipokuwa Dayosisi peke yake.
Hata hivyo Askofu wa
Dayosisi Karagwe Bensoni Bagonza ameeleza utaratibu wote uliofuatwa hadi
wanapata ardhi hiyo ambapo walipewa
tarehe 22 mwezi 12 mwaka 1980 na uongozi wa halmshauri wakati huo ndio
ulisimamia zoezi la kuweka mipaka katika ardhi
Pia
mkuu wa wilaya ya ameagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Karagwe kuanzi
hivi sasa kufanya mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuhakikisha hapaibuki
migogoro mingine ya ardhi isiyokuwa
Post a Comment