Zaidi ya bilioni 10 zimelipwa kwa
kaya 67669 mkoani KAGERA katika hawamu tano katika vijiji 506 mkoani
hapa.
Akisoma taarifa kwa wananchi wa
vijiji vya Kyamukwikwi tarafa Izigo pamoja na kijiji Cha Kabale kata Kagoma
halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkuu wa
mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu SALUM MUSTAPHA KIJUU amesema kuwa
fedha hizo zimesaidia kuwainulia kipato wananchi.
Amefafanua kuwa kutokana na mradi wa
TASAF AWAMU ya tatu kudumu kwa miaka kumi wananchi wanatakiwa
kuzitumia fedha hizo vizuri ambapo amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani
Kagera kusimamia vizuri zoezi la ugawaji pesa kwa wananchi wanaoishi katika kaya
masikini.
Aidha Meja Jeneral Mstaafu Kijuu ametaja changamoto zinazoukabili mradi
wa TASAF 3 pamoja na mambo mengine amesema kuwa baadhi ya wananchi wanatumia
fedha vibaya pindi wanapopata pesa hizo.
Baadhi ya wananchi waliopokea fedha
za mradi wa TASAF katika awamu hizi waliohojiwa na waandishi wa wameonesha
furaha yao.
Post a Comment