SERIKALI mkoani
KAGERA imeteketeza zana haramu za uvuvi zenye ukadirio wa thamani ya
shilingi zaidi ya bilioni moja(1),zilizokuwa zikitumika katika kuvua samaki
katika ziwa Viktoria.
Uteketezaji wa zana hizo umefanywa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu,SALIMU KIJUU ,katika viwanja vya ofisi za halmashauri ya wilaya Muleba,huku akisisitiza yeyote mwenye kujihusisha na vitendo vya uvuvi haramu kuacha mara moja.
Akitoa taarifa juu ya zana hizo Afisa Uvuvi wilaya ya Muleba SYMPHORIAN NGAIZA amesema opereisheni ya kamatakamata zana hizo ilianza miezi mitatu na kufanikiwa kukamata zana hizo ikiwemo Makokoro 192,Timba 10,756,Nyavu ndogo za makila 2,798,kamba za makokoro mita 7,538 na Mitumbwi 161 iliyokutwa inatumiwa na wavuvi haramu.
NGAIZA ametaja zana nyingine kuwa ni Nyavu za dagaa 3,Katuli 12,Samaki kilo 1,688 huku zana zote pamoja zikitajwa kuwa na thamani ya shilingi 1,216,231,280/=ikiwa kama zao la samaki lingefikia kiwango cha kuuzwa kihalali.
Amefafanua kuwa opereisheni hiyo liligharimu kiasi cha shilingi milioni 13,465,000/=zilizotumika kununua mafuta ya Petroli na virainisho,posho ya watumishi na wavuvi walioshirikisha,vibarua na motisha,huku halmashauri ya wilaya Muleba ikichangia 8,900,000/ na kiasi cha shilingi 5,165,000/=ikiwa ni mchango kutoka kwa wavuvi wakubwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu)
KIJUU amewataka wavuvi pamoja na wananchi wote wanaojihusisha na shughuli za
uvuvi haramu mkoani hapa,kuacha tabia hiyo mara moja huku akisisitiza yeyote
atakaye bainika anafanya shughuli hiyo sheria za nchi hazitasita kuchua mkondo
wake.
Post a Comment