Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia
Jenerali Emanuel Maganga amewataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliopo
katika halmashauri zote kutaja kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa mishahara
watumishi hewa 169 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Akiongea na waandishi wa habari,
Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amesema kuwa agizo hilo ni kufuatia agizo la
Mheshimwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kufanya uhakiki wa watumishi
katika halmashauri zote ili kuwabaini watumishi hewa wanaolipwa mishahara
kinyume na utaratibu za utumishi.
Amesema katika hao watumishi hewa
169 waliowabainika wapo ambao walishafukuzwa kazi, wapo ambao wameshafariki na
wengine hawana sifa za kuwa watumishi wa umma.
Maganga amesema kuwa suala la kuwa na wafanyakazi
hewa ni wizi ambao hauwezi kuvumilika na wizi wa kuibia wanyonge hauwezi
kuvumilika.
Amesema kuwa fedha walizokuwa
wakilipwa watumishi hao hewa kwaajili ya mishahara zinatakiwa kurudi zote, pia
wakurugenzi wawafute watumishi hao hewa kwenye orodha ya malipo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa sasa
hivi katika serekali hii ya awamu ya tano hakuna kufanya kazi kwa mazoea.
Post a Comment