ZITTO
KABWE AMTOLEA UVIVU WAZIRI KITWANGA
-------------------------------------------------
Kumekuwa
na maneno yanasemwa na mimi kupuuza katika kipindi cha wiki kadhaa; kwamba
ninapanga kumhujumu Rais Magufuli katika kazi zake. Maneno haya yanaenezwa na
watu wanaotumwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bwana Charles Kitwanga (
nina ushahidi usio na mashaka wa Kitwanga kupanga vijana wa wanaojiita wa UVCCM
kufanya mikutano na waandishi wa habari na anawalipa fedha kufanya hivyo.
Nataka ifahamike bila chenga kama ifuatavyo:
1) Ninamwunga
mkono Rais katika kazi ya kusafisha Nchi. Hii ndio kazi nilikuwa nafanya katika
kipindi cha miaka 10 iliyopita. Nitakuwa mtu wa ajabu sana nisipomwunga mkono
Rais katika vita dhidi ya Ufisadi. Hata hivyo, kamwe sitasita kuweka wazi pale
ninapoona Rais anafanya makosa. Na nimekuwa nikisema wazi wazi na kumkosoa Rais
waziwazi. Lakini pia nimekuwa nikimwambia Rais kwa njia nyengine ambazo
viongozi huwasiliana ninapoona anafanya sivyo. Kukosoa ni kazi moja muhimu sana
na ya kizalendo kuliko lolote ambalo raia anaweza kufanya kwa kiongozi wake.
Kukosoa Serikali ni uzalendo maradufu. Pale panapostahili nitapongeza.
2)
Namsihi Waziri Kitwanga amalize matatizo yake yeye mwenyewe. Yeye kama mmiliki
wa Kampuni ya Infosys yenye mkataba na Serikali katika Wizara anayoongoza sasa
anapaswa aone ni namna gani hana mgongano wa maslahi. Waziri Kitwanga asitafute
watu wa kuwatupia lawama kwenye mambo yanayomhusu. Mimi binafsi sijawahi
kugombana na Charles Kitwanga. Hajawahi kuwa rafiki yangu.
Hajawahi
kuni excite kama Kiongozi ( kimsingi nashangaa mtu kama yeye kuweza hata kuwa
Waziri wa Wizara nyeti kama hiyo) . Zaidi ya yote Waziri Kitwanga sio 'size
yangu'. Kwa protokali za Uongozi, size yangu mimi ni Rais Magufuli, bosi wake.
Naanzaje kuhangaika na Kitwanga? Ili iweje? Namsihi asijipandishe chati kwamba
mimi nataka kumtoa. Ningetaka kumtoa wala asingejua maana ningeshughulika na
aliyemteua. Nasema haya sababu amekaa na Waziri Mkuu na Wabunge kadhaa
akilalamika kuwa nataka kumtoa Uwaziri. Asinipe dhambi, Uwaziri atatolewa na
aliyemteua kwa madhambi aliyofanya. Asitafute bangusilo!
3)
Mimi kwa wiki kadhaa sasa nipo nje ya Nchi ( nchini Marekani katika Chuo
Harvard kwa masomo) . Sijui na sihusiki na njama zozote dhidi ya yeyote. Kwanza
hizo sio aina ya siasa ninazofanya. Siasa ninazofanya ni Siasa za Maendeleo ya
Wananchi na sio Siasa za kuwinda watu.
4)
licha ya kuwa Kiongozi wa Chama, Mimi ni Mbunge wa Chama Cha ACT Wazalendo. Kwa
hiyo nafuata maelekezo ya chama changu katika kazi zangu. Chama changu katika
Mpango Mkakati wake kimeniagiza kufanya Siasa za Maendeleo. Chama changu
kinaunga mkono juhudi zote za Rais kurejesha imani ya wananchi kwa Serikali kwa
kupambana na ufisadi.
Hata
hivyo Chama Cha ACT Wazalendo kinamtaka Rais ajenge mfumo imara wa kitaasisi
ili mapambano dhidi ya ufisadi yawe endelevu. Hivyo, porojo za kwamba nataka
kumwangusha Rais ni porojo za watu wasionijua binafsi na wasiojua misingi ya
ACT Wazalendo
5)
Nawasihi Watanzania wote a) kumdharau Waziri Kitwanga na kumtaka ajibu tuhuma
zinazomkabili za Kampuni yake binafsi kufanya kazi na Idara katika Wizara
anayosimamia na kwamba ajipime kama anatosha kuendelea kumsaidia Rais kazi b)
kuendelea kumwunga mkono Rais katika vita dhidi ya ufisadi.
Kama
nilivyosoma mwaka jana ' asiyemwunga mkono Magufuli yupo upande wa mafisadi' c)
kuepuka siasa za porojo zinazoendeshwa na vijana wanaotafuta nafasi za
kuteuliwa na d) kutaka umadhubuti wa kila jambo linasomewa ili kuepuka kuonea
watu.
Zitto
Kabwe.
Post a Comment