Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WATAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU SIKU YA UTAMADUNI DUNIANI KWA KUCHANGIA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi  wametakiwa  kuitikia  wito  wa   kushiriki  kikamilifu  siku  ya  wiki  ya  utamaduni kwa  kuanzia  katika  maandalizi...




Wananchi  wametakiwa  kuitikia  wito  wa   kushiriki  kikamilifu  siku  ya  wiki  ya  utamaduni kwa  kuanzia  katika  maandalizi  ili  kufanikisha  siku  hiyo  muhimu na  wametakiwa  kuchangia chochote  walichobahatika  kupata   pia  kuandaa  mali  kale za  kuonesha  kwenye  wiki  ya  utamaduni  itakayoanza  Mei 13  hadi  mei 21  ambayo  ni  kilele.


Wito  huo  umetolewa  katika  kikao  cha  maandalizi  ya  wiki  ya  utamaduni  kilichofanyika  Nyakahanga  ofisi  ya  Kata  maarufu  kama  arukiko wajumbe  wamesema  ili  shughuli  na  wiki  ya  utamaduni  ifanikiwe  ni  lazima  wananchi  kushiriki  kikamilifu  kwa  kila  hatua.


Katibu  wa  kamati  ya  maandalizi  Aloyce  Mjungu  ambaye  pia  ni  Afisa  Utamaduni  wilaya  ya  Karagwe  amewaambia  wajumbe  wa  kikao  hicho  cha  maandalizi  ya  siku  ya  utamaduni  kuwa tayari  barua  zilizosainiwa  na  Katibu  Tawala  wilaya  ya  Karagwe  Mustaph  Said  kuwa  zimeishatumwa  kwa  wadau  na  wengine  wameanza    kuitikia  kwa  kuchangia   hivyo  akasema  nguvu  zaidi  inahitajika  kuwakumbusha  wengine  waliopokea  barua  hizo  ila  na  wananchi  wanatakiwa   kuchangia  kwani  suala  la  utamaduni  ni  wa  kila  mtu.



Wajumbe  wa  kikao  hicho  wakijadili  agenda  mbalimbali  katika  kikao  hicho  wamebainisha  kuwa   nguvu  ya  pamoja  na  ushirikiano,umoja  na  mshikamano  ni  muhimu  katika  kipindi  hiki  cha  maandalizi  ili  wiki  ya  utamaduni  iwezekufanikiwa  zaidi  na  kusaidia  kuelimisha  jamii  kutambua  masuala  muhimu  kwenye  maisha  yao  ya  kila  siku.

Mwenyekiti  wa  kikao  hicho Mtume   mstaafu  Mathias  Nzarombi  amesema   kupitia  kuadhimisha  wiki  ya  utamaduni  iwe fundisho  kwa  kizazi  cha  sasa  kutambua,kuthamni  na  kuhifadhi  utamaduni  wao  kwa  ajili  ya  kizazi  cha  sasa  na  kijacho  hivyo  kutoa  mwanga  kwa  jamii.

Hata  hivyo  kikao  hicho  kiliunda  kamati  tisa  na  kupanga  wajumbe  wake  na  wenyeviti  wa  kamati  hizo  ikiwa  ni  mmoja  ya  mkakati  wa  kufanikisha  siku  hiyo  ambayo  ni  muhimu  kwa  kumbukumbu  za  utamaduni  pia  wageni  toka  nje  ya  nchi  wanatarajia  kuhudhuria  wiki  ya  utamaduni  likiwemo  na  shirika  la  Umoja  wa  mataifa  linalijishughulisha  na  elimu,sayansi  na  utamaduni  yaani UNESCO .

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top