Vyama vinavyounda umoja wa Katiba UKAWA wamesema hawatachangia bajeti yoyote ile ya wizara mpaka pale serikali itakaporuhusu kurushwa moja kwa moja matangazo hayo (LIVE)uamuzi huo umetangazwa leo baada ya utaratibu uliokuwepo zamani ya kila mwandishi kuingia Bungeni akiwa na vifaa vyake vya kazi na kurekodi matukio muhimu anayoona ni habari lakini nao umefutwa na badala yake wanapewa matukio yaliyorecodiwa na uongozi wa Bunge ndiyo watangaze hayo.
Awali serikali ilisema shirika la utangazaji Tanzania halitanguwa linarusha moja kwa moja (LIVE)kwani wanabana gharama za matangazo lakini vyombo binafsi vilikubali kurusha kwa gharama zao lakini awamu hii vimebanwa na badala yake uongozi wa Bunge ulitangaza mfumo mpya kuwa watakuwa na studio yao maarufu ambayo vyombo vyote vitapata kutokea hapo.
Mfuko wa kufadhili vyombo vya habari na waandishi wa habari(TANZANIA MEDIA FOUNDATION(TMF) walisema wako tayari kutoa pesa kugharimia matangazo hayo ili wananchi waweze kupata kufuatilia kinachoendelea kwa chombo hicho muhimu cha kutunga sheria na cha wawakilishi wa wananchi hapa nchini mpaka sasa serikali haijawahi kutoa majibu juu ya ombi hilo.
Post a Comment