HOTUBA
YA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB) MHESHIMIWA FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB)
AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO
YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MWAKA WA FEDHA
2016/17.
Inatolewa
chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo
la Januari, 2016
_________________________________
1.
SHERIA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MAWAZIRI (MINISTERS – DISCHARGE OF
MINISTERIAL FUNCTIONS – ACT, 1980.
Mheshimiwa
Spika, kifungu cha 5(1) kinaweka masharti kwa Rais kutengeneza mwongozo wa
muundo na utekelezaji wa majukumu ya Serikali yake.
Inasomeka
ifuatavyo: Nanukuu “the President shall from time to time by notice published
in the Gazette, specify the departments, business and other matters and
responsibility for which he has retained for himself or he has assigned under
his direction to any minister and may in that notice specify the effective date
of the assumption of that responsibility…….” mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa
Spika, mpaka sasa Serikali inafanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji wake
na kazi kwa wizara mbalimbali. Hii ina maana kwamba Serikali inafanya kazi kwa
kauli za Rais na Mawaziri bila kufuata mwongozo wowote wenye msingi na uhalali
wa kisheria.
Mheshimiwa
Spika, mpaka sasa mwongozo wa utendaji wa Serikali kwa kila Wizara (Instrument)
unaotumika ni ule uliochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 494A la tarehe
17/12/2010. Kwa mujibu wa Instrument hiyo, majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni:
Coordination of Government Business
Leader of Government Business in the National
Assembly
Link between Political Parties and Government.
National Festivals and Celebration of
Management of Civic Contingencies (relief).
Facilitation and Implementation of Plans for
the Development of Dodoma as Capital of Tanzania.
Coordination and Supervision of Transfer of
the Government to Dodoma.
Government Press Services.
Investment, Economic Empowerment,
Public-Private-Partnership (PPP), Poverty alleviation Policies and their Implementation.
Facilitation of the Development of Informal
Sector.
Performance Improvement and Development of
Human Resources under this Office
Extra – Ministerial Department, Parastatal
Organisations, Agencies, Programmes and Projects under this Office.
REGIONAL
ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT:
Decentralization by Devolution (D by D), Rural
Development, Urban Development Policies and their Implementation.
Regional Administration.
Primary and Secondary Education Administration
Dar Rapid Transit – DART.
Performance Improvement and Development of
Human Resources under this Office.
Extra-Ministerial Departments, Parastatal
Organisations, Agencies, Programmes and Projects under this Office.
Mheshimiwa
Spika, kitendo cha Serikali hii kuendesha kazi zake kwa Mwongozo wa 2010 ina
maanisha kwamba majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu bado ni yale yale
yaliyochapishwa mwaka 2010, kwa sababu gazeti hilo la Serikali halijafutwa.
2.
UVUNJWAJI WA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KUHUSIANA NA BAJETI UNAOFANYWA NA
SERIKALI
Mheshimiwa
Spika, hili ni Bunge la Bajeti ambalo kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(b) ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepewa mamlaka ya kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano
wa Bunge wa kila mwaaka wa Bajeti kwa madhumuni ya kujadili na kuidhinisha
Bajeti ya Serikali.
Mheshimiwa
Spika, Ikiwa fedha zilizoidhinishwa na
Bunge hazikutosha kutekeleza majukumu ya Serikali , kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 kinaelekeza kwamba: “ Serikali itawasilisha
Bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo zimezidi
kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa madhumuni ya kugharamia mahitaji
ambayo hayakupangwa”.
Mheshimiwa
Spika utaratibu huu unatiliwa nguvu na Sheria ya Fedha za Umma wa mwaka 2001( Public Finacne Act,
2001)ambapo kifungu cha 18 (3) na (4) kinaitaka Serikali kuleta Bungeni bajeti
ya nyongeza ( mini-budget) kwa ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha
zilizoidhinishwa awali hazikutosha.
Mheshimiwa
Spika, utaratibu huo wa kisheria ume kuwa
ukivunjwa na Serikali kwa kufanya
matumizi ya fedha ambazo hazikuidhinishwa na Bunge jambo ambalo linaua dhana ya
madaraka ya Bunge ya kuisimamia na kuishauri Serikali.
Mheshimiwa
Spika, ili kuthibitisha jambo hilo, kwa mfano bajeti ya maendeleo iliyokuwa
imeidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka
wa fedha 2015/16 ilikuwa ni shilingi
bilioni 883.8 ambapo kati ya fedha hizo,
fedha za ndani zilikuwa ni shilingi bilioni 191.6
Mheshimiwa
Spika, Jambo la kushangaza ni kwamba hadi kufikia mwezi Machi 2016 Wizara
ilikuwa imeshapokea kutoka hazina shilingi
bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za
ndani.
Mheshimiwa
Spika, ukitazama takwimu hizo utaona kuwa kuna ongezeko la fedha zilizotolewa
na hazina hadi kufikia mwezi Machi 2016 ukilinganisha na fedha zilizoidhinishwa
na Bunge. Tangu kuidhinishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, hakuna bajeti ya
nyongeza iliyoletwa Bungeni na Serikali kwa ajili ya kupata idhini kutokana na matakwa ya Sheria ya Bajeti ya
2015 au sheria ya Fedha ya 2015.
Mheshimiwa
Spika, kitendo cha Serikali kuamua kufanya re-allocation ya bajeti bila kupata
idhini ya Bunge ni dharau kwa bunge lakini mbaya zaidi ni uvunjaji wa Katiba na
Sheria.
3.
UHURU NA MADARAKA YA MHIMILI WA BUNGE
Mheshimiwa
Spika, Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalitaja
Bunge kuwa ndicho chombo kikuu katika Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na
madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Katika hali
isiyo ya kawaida, kifungu hiki cha Katiba kimevunjwa na badala yake Serikali
imelipoka bunge madaraka yake na Bunge kwa maana ya uongozi wake wanaonekana
kushiriki na kukubali kupokwa huku kwa madaraka na uhuru wake.
Mheshimiwa Spika, Bunge ni chombo cha
uwakilishi wa wananchi, na wananchi wana haki ya kujua Bunge lao linavyofanya
kazi ili wawe na uwezo wa kuwawajibisha wawakilishi wao iwapo hawafanyi kazi
inavyostahili. Katika hali isiyo ya
kawaida, Serikali na uongozi wa Bunge, imewapoka wananchi haki yao ya kupata
habari za Bunge kwa kuzuia mijadala Bungeni kurushwa moja kwa moja na
televisheni ya Taifa na vyombo vingine vya habari vya kujitegemea.
Mheshimiwa
Spika, Jambo hili pia ni uvunjwaji wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, ambayo inasema kwamba kila mtu anao uhuru wa kuwa na
maoni na kueleza fikra zake; anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari
bila ya kujali mipaka ya nchi; anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya
kutoingiliwa katika mawasiliano yake na anayo haki ya kupewa taarifa wakati
wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na
pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii,
Mheshimiwa
Spika, katika Mazingira kama hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haiko tayari
kuendelea kushiriki uvunjaji wa Katiba Sheria na haki za msingi za wananchi.
Mheshimiwa
Spika, Kambi rasmi ya Upinzani haitakuwa tayari kuwasilisha hotuba yake katika
mazingira haya na inaushauri uongozi wa Bunge kupata ufumbuzi wa haraka wa
kadhia hii ili kurejesha heshima ya Bunge na haki za msingi za wananchi. Hivyo
basi Kambi bado inatafakari kwa kina na makini hatua za kufuata.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Freeman
Aikaeli Mbowe (Mb)
KIONGOZI
WA UPINZANI BUNGENI PIA
MSEMAJI
MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
KATIKA
OFISI YA WAZIRI MKUU
22
Aprili, 2016.
Post a Comment