Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: CCM YAWAKUMBUKA WANAFUNZI KWA KUTOA ZAWADI NA MABALOZI PIA NAO WAKUMBUKWA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
  Jumuia   ya   wazazi   ya   chama   cha   Mapinduzi   (CCM)imetoa   msaada   wa   madaftari,kalamu   na   sabuni   kwa   wanafunzi  ...
 
Jumuia  ya  wazazi  ya  chama  cha  Mapinduzi  (CCM)imetoa  msaada  wa  madaftari,kalamu  na  sabuni  kwa  wanafunzi  wanaoishi  katika  mazingira  magumu  wanaosoma  katika  shule  za  msingi  za  Lukole  na  Karalo  ambao  wanafanya  vizuri  darasa  wametoa  zawadi  hiyo  katika  siku  ya  kilele cha  wiki  ya  wazazi  ambayo  kwa  wilaya  ya  Karagwe  imefanyika  viwanja  vya  ccm  kata  ya  IHANDA.



Zawadi  hizo  zimekabidhiwa  na  mwenyekiti  wa  jumuia  ya  Wazazi (CCM) wilaya  ya  KARAGWE  Exsavery   Buguzi  ambaye  pia  ni  diwani  wa  Kata  ya  Nyakakika  amesema  kuwa  wao  kama  wazazi  wanatambua  watoto  wenye  mahitaji hivyo  wameamua  kutoa  zawadi  kwa  wanafunzi  15  kila  shule  kwa  wale  tu  wanaofanya  vizuri  darasani  lakini  hawatakomea  hapo  kwani  wanatambua  uwepo  wa  wanafunzi  wengine,pia  mabalozi  wa  CCM  katani  Ihanda  nao  wamepatiwa  zawadi  pamoja  na  kuwatembelea   kwenye  makazi  yao  lengo  ni  kutambua  mchango  wao  walioutoa  kwa  kipindi  cha  kampeini  za  uchaguzi  mkuu  wa  mwaka  jana  na  kukisaidia  chama  hicho  kuibuka  na  ushindi.


Akihutubia wananchi  na  wanacha wa  chama  hicho Mwenyekiti  wa  Chama  cha  Mapinduzi  CCM Wilaya  ya  Karagwe  Robson  Mtafungwa  ambaye  alikuwa mgeni  rasmi  katika  kilele  cha  wiki  ya  wazazi  wilayani  Karagwe  amesema  wakati  wa  malumbano  ya  kisiasa  umeisha  kilichobakia  ni  kuwaamini  viongozi  waliopatikana ili waweze  kuwatumikia  kwa  kutekeleza  wale walichowaahidi  wananchi.
 
Amesema  kuwa Rais  Magufuli  ameonesha  njia  kwa kuwatumikia  watanzania  bila  kujali  itikadi  za  vyama  vyao  kwani  wananchi  walimkabidhi  mamlaka  kuwatumikia  na  ndiyo  maana  katika  falsafa  yake  ya  kutumbua  majipu  anatumbua  wanaccm  na  wasiyokuwa wanaccm.

 
Naye  katibu  wa jumuia  IDD MVANO akitoa  maelezo  kwa  wanachama  na  wananchi  amesema  katika  kusherekea  wiki  ya  wazazi  wameamua  kufanya  shughuli  kadhaa  kwa  kutembelea  mabalozi  pia  kutoa  zawadi  kwa  wanafunzi  ambao wanaishi  katika  mazingira  magumu  na  wanafanya  vizuri darasani  kwa kutambua  umuhimu wa wazazi kwa  watoto.


Jumuia ya  wazazi  ya  chama  cha  mapinduzi  CCM ni  moja  ya  jumuia  muhimu  zinazounda  chama  hicho  na  huwa  na  shughuli  za  wiki  ya  wazazi  kila  mwaka  na  kilele  chake  kitaifa  mwaka  huu   zitafanyika  mkoani Morogoro.

Hata  hivyo  kivutio  kikubwa  katika mkutano  wa  jumuia  ya  wazazi  ya  CCM uliofanyika  kijiji  cha  Lukole  alikuwa  ni  mwenyekiti  wa  kijiji Prisca  Bosco  pamoja  na  mwenyekiti  wa  kitongoji  Bosco  Kanyomoza  ambao  wote  wanatokana  na  chama  cha  demokrasia  na  maendeleo CHADEMA walihudhuria  mkutano  huo  pia  hao  ni  mme  na  mke  ambapo  mwananke  ni  mwenyekiti  wa  kijiji na  mwanaume  ni  mwenyekiti  wa  kitongoji.
07 Apr 2016

About Author

Advertisement

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top