Wananchi wameaswa
kuhakikisha usalama wa mali zao na watu wengine na kutoa taarifa pale waonapo
mali wasizofahamu mmiliki wake katika vyombo husika vya sheria.
Kauli hiyo imetolewa na
mwenyekiti wa Kitongoji Nyakashambya Kijiji cha Nyabwegira Kata ya Ngama
Wilayani Karagwe Laiton John Mlaki wakati akiongea na chombo hiki baada ya
wananchi katika kitongoji chake kuokota Ng’ombe wawili mali ya Anthony Elias
Kahigwa mkazi wa Chanika.
Aidha ameushukuru mtandao huu kwa uharaka wake katika
kuhakikisha matangazo ya muhimu yanapewa kipaumbele ili kusaidi wahusika
kufanikisha mahitaji yao.
Kwa upande wake Anthony
Elias Kahigwa ambaye alipotelewa na Ng’ombe wake hao ameelezea pia umuhimu wa
Redio na jinsi alivyopata mafanikio katika matukio tofauti aliyoyapata na
kutumia Redio.
Pia amewaasa wananchi
wengine kuiga mfano wa wananchi waliotoa taarifa za kupatikana kwa Ng’ombe wake
kwa kuzingatia kuwa ni hatua ya uaminifu na usalama katika jamii.
Ng’ombe hawa wamepotea jana
majira ya asubuhi na kupatikana majira ya mchana baada ya kukamatwa na wasamalia
wema wakiwa wanalanda landa bila kuwa na mchungaji.
Kumekuwa na matukio ya
kuibiwa na kupotea Ng’ombe katika Wilaya
ya Karagwe ambapo wengine wamekuwa
wakipatikana huku wengine kutopatikana.

Post a Comment