Rai hiyo imetolewa na datari wa idara ya upasuaji katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera, Dk. MARTINE RWABILIMBO, wakati akizungumzia zoezi la ujio wa madaktari bingwa waliofika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kufanya upasuaji wa watu wenye midomo sungura, vidonda ndugu na makovu.
Dk. RWABILIMBO amesema kuwa pamoja na huduma hiyo kutolewa bure na kufanyika hamasa ya kutosha, bado idadi ya watu waliojitokeza ni ndogo na kuwa sio kwamba wagonjwa wenye uhitaji huo hawapo bali hali hiyo inatokana na watu kuendelea kuwaficha wagonjwa hasa wenye ulemavu majumbani.
Amefafanua kuwa walikuja madaktari bingwa wawili wakiwa na wauguzi wawili kutoka nchini Uholanzi, wakiwa na lengo la kufanyia upasuaji angalau wagonjwa 30 lakini waliofanyiwa ni 18 tu, na kuwa walifika hospitalini hapo Machi 22 na walipaswa kukamilisha kazi hiyo Aprili mosi mwaka huu lakini kutokana na kukosa wagonjwa walifunga kazi Machi 30.
Amebainisha kuwa lengo la madaktari bingwa kutoka nje kufika hospitalini hapo, pamoja na kufanyia wagonjwa upasuaji pia wanasaidia kuwaongezea ujuzi madaktari wanaokuwa katika hospitali husika, ili hata kama hawapo huduma za namna hiyo ziweze kuendelea.
.Akizungumzia zoezi hilo mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji Jonathan Andrew mkazi wa Kyaka wilaya ya Missenyi ameshukuru kwa huduma aliyoipata bure maana awali alifika katika hospitali ya Ndolage iliyoko wilayani Muleba na kuambiwa ili kufanyiwa upasuaji wa kidonda kilichomsumbua zaidi ya miezi saba inabidi atafute shilingi 200,000.
Kati ya wagonjwa 18 waliofanyiwa upasuaji huo, watu wazima ni watatu na watoto ni 15.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.