Kufuatia kilio cha muda
mrefu kwa watu wenye ualbino kuhitaji kupatiwa huduma ya matibabu bure bila
mafanikio shirika lisilokuwa la
kiserikali la Standing Voice lenye makao yake Mkoani Mwanza limejitolea
kuwasaidia mafuta ya Ngozi na ukaguzi wa Afya ya Kansa ya Ngozi katika Baadhi
ya Vituo vya Afya vya Kanda ya Ziwa.
Hayo yamethibitishwa na
Katibu wa chama cha watu wenye Ualbino Mkoa wa Kagera Ignas Lugemalira na
kubainisha vituo vya Afya vitakavyotoa huduma hiyo kwa Mkoa wa Kagera pamoja
nawilaya zitakazohusika.
Lugemalira amekieleza chombo
hiki kuwa hatua hii imekuja baada ya kuangaika kwa muda mrefu bila kupata
matokeo chanya juu ya hatma ya Afya ya watu wenye ualbino.
Aidha ameeleza kusikitishwa
na ahadi za serikali zisizotekelezeka na kwamba bado watu wenye ualbino
hawajapewa kipaumbele katika nchi yao kama yalivyo makundi mengine.
Amesema zoezi hili ni
mwendelezo huku akitaja kukabiliwa na changamoto ya mahudhurio hafifu ya watu
wenye ualbino kutokana na Halmashauri za wilaya husika kushindwa kuwasafirisha
kwenda kupata huduma katika vituo vilivyotajwa.
Lugemalira ameiomba jamii
pamoja na serikali ya Tanzania kutoa ushirikiano kwa watu wenye Ualbino
kuhakikisha wanafikiwa huduma kama zinavyokuwa zikitolewa kwani wanastahili
kupata haki zao za msingi kama yalivyomakundi mengine.

Post a Comment