Idadi ya Wazee na watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi wilayani Muleba mkoani Kagera imeongezeka
kutoka 427 kwa mwaka 2014 /2015 hadi 615 kwa mwaka 2015/2016.
Akizungumza na Karagwe Forum kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Muleba
FRANSINS MTINGA amesema ongezeko hilo ni kubwa sana katika wilaya hiyo.
Amebainisha kuwa kwa sasa watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi ni 572 ikiwa wazee wanaoishi katika
mazingira hatarishi wilayani humo ni 43.
Aidha mtinga ametoa wito kwa
wadau mbalimbali wilayani humo kuwasaidia wazee hao na watoto kwa kuwapatia
maladhi na chakula pamoja na misaada mingine.
Hata hivyo ametaja sababu kubwa
zinazosababisha ongezeko la watoto kuishi katika mazingira hatarishi au wazee
kuwa ni pamoja na kuwapoteza ndugu zao wenye uwezo,mifarakano katika ndoa
pamoja na upendo kupungua kwa baadhi ya familia.
Post a Comment