MCT
yatangaza majina ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania
(EJAT) 2015
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tom Nyanduga kuwa Mgeni Rasmi
Kamati
ya maandalizi ya EJAT 2015 leo limetangaza majina 84 ya wateule wa Tuzo za
Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015. Idadi hiyo ni ongezeko la
wateule 31 ukilinganisha na tuzo za 2014 ambapo wateule walikuwa ni 53 tu.
Pia
kamati imeeleza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
Tom Bahame Nyanduga ndio Mgeni Rasmi kwenye Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa
Habari Tanzania (EJAT ) 2015
zitakazofanyika kwenye tamasha la usiku la utoaji wa tuzo hizo Aprili 29, 2016 , Dar es Salaam.
Kutangazwa
kwa wateule wa EJAT 2015 kunafuatia kukamilika kwa kazi ya kuzipitia na
kuchagua zile zilizo na ubora zaidi iliyofanywa na jopo la majaji 10 lililokaa
mwezi Machi mwaka huu. Majaji hao ambao ni wataalamu mbalimbali wa masuala ya
habari walipitia kazi za kiandishi zaidi ya 570 zilizowasilishwa kwenye makundi
ya kushindaniwa 22 kwenye tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT)
2015.
Ripoti
ya jopo la majaji hao kuhusu wateule wa EJAT 2015, inaonyesha kuwa kumekuwa
na ongezeko kubwa kwa wateule kwa
upande wa luninga ambapo kuna wateule 27
kutoka wateule wawili katika tuzo za 2014. Pia kuna ongezeko kwenye wateule wa
redio kutoka 17 hadi 27. Hata hivyo kwa upande wa magazeti wateule wamepungua
kidogo kutoka wateule 34 wa tuzo za 2014 hadi 32 kwa tuzo za mwaka 2015.
Idadi
ya wateule wanawake pia imeongezeka kufikia 28 kutoka wateule 18 kwenye tuzo za
EJAT 2014. Pia ripoti inaonyesha
kuongezeka kwa kazi zilizoletwa na redio za kijamii mwaka huu ambapo baadhi yao
zimeweza kutoa wateule kwenye tuzo za EJAT 2015.
Jopo
hilo la majaji liliongozwa na mwenyekiti wake, Bi. Valerie Msoka, wajumbe
wengine walikuwa Dk. Joyce Bazira Ntobi
ambaye alikuwa katibu wa jopo, na Ali
Uki. Wanajopo wengine walikuwa Jesse
Kwayu, Kiondo Mshana, Juma
Dihule, Godfrey Nago, Nathan Mpangala
na Pili Mtambalike. Waandishi hao 84
wataingia kwenye kinyanganyiro cha mashindano ya EJAT 2015.
Majaji
hao 10 waliapishwa na Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas
Mihayo Machi 11, 2016 kabla ya kuanza
kazi hiyo. Hii itakuwa ni mara ya saba
kuwatuza waandishi waliofanya vizuri katika kazi zao za kiuandishi chini ya
utaratibu wa EJAT.
Sambamba
na EJAT, Jopo la wataalam kwa ajili ya Tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika
Uandishi wa Habari (LAJA) umeanza kazi ya kutafuta mteule wa tuzo hiyo kwa
mwaka huu ambae atatangazwa wakati wa Tamasha hilo la usiku. Jopo la LAJA linalongozwa na Mwenyekiti wake
Bi. Lilian Kallaghe lina wajumbe watano ambao ni pamoja na Hamis Mzee, Fili
Karashani, Joseph Kulangwa na Wenceslaus Mushi.
Makundi
yaliyoshindaniwa ni yafuatayo:
1.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi na Biashara
2.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na Utamaduni
3.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Mazingira
4.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya
5.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za VVU/Ukimwi
6.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watoto
7.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utawala Bora
8.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia
9.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi na Teknolojia
10
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi
11.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya ya Mama na Mtoto
12.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu
13.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi
14.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watu Wenye Ulemavu
15.
Mpiga Picha Bora Magazeti
16.
Mpiga Picha Bora Runinga
17.
Mchora Katuni Bora
18.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo
19.
Tuzo ya Afya ya Uzazi kwa vijana
20.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini
21.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Manunuzi ya Umma
22.
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kodi na Ukusanyaji Mapato
Ifuatayo
ni orodha ya wateule wa EJAT 2015 ambao wanatoka kwenye vyombo mbalimbali vya
habari
WATEULE
WA EJAT 2015
SN
JINA
LA MWANDISHI
CHOMBO
CHA HABARI
MKOA
ANAOTOKA
Sylvester
Joseph
Afya
Radio
Mwanza
Fatuma
Mtengamani
Ulanga
FM
Ulanga-Mahenge
(M orogoro)
Adam Hhando
CG FM
Tabora
Abisae Maeda
TV1/Kilimanjaro Film Institute
Arusha
Mwashamba Juma
Zanzibar Leo
Zanzibar
Jackline Masinde
Mwananchi
DSM
Peter Rodgers
ITV
Mwanza
Lucas Maziku
Star TV
Mwanza
Maajabu Madiwa
Pangani FM
Pangani-Tanga
Ezekiel Kamanga
BBC & Bomba FM
Mbeya
Malongo Mbeho
Metro FM
Mwanza
Annastazia Maginga
Raia Tanzania
Mwanza
John Leon Lewanga
TBC
DSM
Mussa Kinkaya
Sunrise FM
Arusha
Victor Makwawa
Dodoma FM
Dodoma
Pili Mlindwa
Pangani FM
Pangani-Tanga
Zulfa Golay
Mwananchi
Arusha
Tumaini Msowoya
Mwananchi
Iringa
Nuzulack Dausen
The Citizen
DSM
Haji Mohamed
Zanzibar Leo
Pemba-Zanzibar
Silvano Kayera
Mlimani
DSM
Christian Msafiri
CG FM
Tabora
Grace Mbise
Bomba FM
Mbeya
Salome Kitomari
Nipashe
DSM
Kelvin Matandiko
Mwananchi
DSM
Mansour Jumanne
SAUT FM
Mwanza
Frank Bahati
TBC1
DSM
Khamis Suleiman
Channel Ten
DSM
Emmanuel Buhohela
ITV
DSM
Lusekelo Philemon
The Guardian
DSM
John Nsuza
TV1
Arusha
Esther Zelamula
Channel ten
DSM
Elibahati Akyoo
TV1/ Kilimanjaro Film Institute
Arusha
Idd Juma
Afya Radio
Mwanza
Mashaka Mgeta
The Guardian
DSM
Kisali Simba
Star TV
Shinyanga
Editha Kinyaiya
TV1/Kilimanjaro Film Institute
Arusha
Emmanuel Kitomari
TV1/Kilimanjaro Film Institute
Arusha
Maulid kambaya
Radio One
DSM
Lulu George
Nipashe
Tanga
Mussa Siwayombe
Mwananchi
Arusha
Victor Eliah
TBC
DSM
Cassius Mdami
Channel Ten
DSM
Anthony Masai
Triple A FM
Arusha
Temigunga Mahondo
Radio Country FM
Iringa
Beatrice Shayo
Nipashe
DSM
Rahma Suleiman
Nipashe
Zanzibar
Haika Kimaro
The Citizen
DSM
Halfan Lihundi
ITV
Arusha
Lydia Igarabuza
EATV
DSM
Valeria Mwalongo
Tumaini
DSM
Peninah Kajura
HHC Radio
Mwanza
Goodluck Mvamba
SAUT FM
Mwanza
Said Michael
Mtanzania
DSM
Abdul Kingo
Nipashe
DSM
Nora Damian
Mtanzania
DSM
Sauli Gilliard
The Citizen
DSM
Alfayo Misiyeki
TV1/Kilimanjaro Film Institute
Arusha
Samson Kapinga
TV1/ Kilimanjaro Film Institute
Arusha
Florence Majani
Mwananchi
DSM
Selemani Mkufya
TBC1
DSM
Kasilda Mgeni
Star TV
Morogoro
Tuma Dandi
Mlimani
DSM
Eveline Mhozya
CG FM
Tabora
Vivian Pyuza
CG FM
Tabora
Joseph Mwendapole
Nipashe
DSM
Hadija Jumanne
Mwananchi
DSM
Christina Mwakangale
Nipashe
DSM
Sanula Athanas
Nipashe
DSM
Mwanahiba Richard
Mwanaspoti
DSM
Japhary Ramadhan
ABM FM
Dodoma
Bernard Lugongo
The Citizen
DSM
Emmanuel Mollel
TV1/ Kilimanjaro Film Institute
Arusha
Joel Ulomi
Arusha One
Arusha
Haji Nassor
Zanzibar Leo
Chake Chake-Pemba
Peti Siyame
Habari Leo
Sumbawanga-Rukwa
Robert Okanda
Dailynews
DSM
Nuru Hassan
Afya
Mwanza
Shija Felician
The Citizen
Kahama
Salum Maige
Mwananchi
Geita
Projestus Binamungu
Star TV
Mwanza
Regina Kulindwa
Afya
Mwanza
Denis Nyali
Nuru
Iringa
Sam Mahela
ITV
DSM
Waandaaji wa EJAT 2015 ni pamoja na
Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini
mwa Afrika- Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri (TEF), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya
Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Chama cha
Waandishi wa Habari Walio katika Mapambano Dhidi ya UKIMWI Tanzania (AJAAT),
Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), PSI-Tanzania,
Unicef, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Haki Elimu, SIKIKA, Evidence
for Action, Amref Health Africa na BESTDialogue/ANSAF.
Kajubi D. Mukajanga
Mwenyekiti
Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2015
Idadi ya Wazee na watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi wilayani Muleba mkoani Kagera imeongezeka
kutoka 427 kwa mwaka 2014 /2015 hadi 615 kwa mwaka 2015/2016.
Akizungumza na Karagwe Forum kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Muleba
FRANSINS MTINGA amesema ongezeko hilo ni kubwa sana katika wilaya hiyo.
Amebainisha kuwa kwa sasa watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi ni 572 ikiwa wazee wanaoishi katika
mazingira hatarishi wilayani humo ni 43.
Aidha mtinga ametoa wito kwa
wadau mbalimbali wilayani humo kuwasaidia wazee hao na watoto kwa kuwapatia
maladhi na chakula pamoja na misaada mingine.
Hata hivyo ametaja sababu kubwa
zinazosababisha ongezeko la watoto kuishi katika mazingira hatarishi au wazee
kuwa ni pamoja na kuwapoteza ndugu zao wenye uwezo,mifarakano katika ndoa
pamoja na upendo kupungua kwa baadhi ya familia.
Post a Comment