Jeshi la polisi mkoani KAGERA limewaagiza wananchi wote na
makampuni binafsi wanaomiliki silaha bila kufuata taratibu na sheria
kusalimisha silaha zao katika kituo cha polisi au ofisi za vijiji na mitaa.
Akizungumza na waandishi wa habari wa kamanda wa jeshi la polisi mkoani KAGERA
AGUSTINI OLLOMI amesema kuwa zoezi hili linawahusu wananchi wote wanaomiliki
silaha pamoja na makampuni binafsi yanayomiliki kinyume na sheria.
Amefafanua kuwa zoezi hili limetangazwa na serikali hivyo
wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria inabidi wazisalimishe hivyo
ametumia kuwaomba wananchi wasalimishe silaha hizo kwa hiari yao wenyewe kabla
hatua kali za kisheria hazijachukuliwa.
Aidha amewataka wale wote ambao ndugu zao wametangulia mbele ya
haki kama wameacha silaha kutafuta mirathi
yao ili kuzipeleka silaha hizo
katika kituo cha polisi ili zitambuliwe.
Hata hivyo OLLOMI amewataka wananchi kuwafichua wale wote ambao
wanamiliki silaha ambao hawatakuwa tayari kusarimisha silaha zao kwa hiari
katika vijiji na mitaa au kituo cha polisi ili wachukuliwe hatua kali za
kisheria.
Zoezi la kuhakiki silaha mkoani KAGERA litaanza rasmi April MOJA
hadi Juni 30 mwaka huu lengo ikiwa ni
kujua idadi ya wananchi wanaomiliki silaha mkoani KAGERA.
Post a Comment