Wazee Wilayani Karagwe
wameiomba serikali kufuatilia utekelezaji wa sera ya matibabu bure kwa wazee
katika baadhi ya vituo vya Afya na zahati Hapa nchini ili kuwawezesha kupata
huduma ya Afya inayostahili.
Wakizungumza na KARAGWE FORUM
baadhi ya wazee wa kijiji cha Rwambaizi
kata ya Kanoni hapa wilayani Karagwe wamesema kuwa pamoja na sera
kutamka kuwa wazee wapate huduma ya matibabu bure lakini bado wanatumia gharama
zao kupata matibabu katika vituo vya Afya na Zahanati nap engine kuagizwa
sehemu ya kwenda kununua dawa.
Mzee Venant Dio Rukehata
mwenye Umri wa miaka 81 ameelekeza kilio chake kwa Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto
kuhakikisha wazee wanapata matibabu bure kama
sera inavyoelekeza.
Kwa upande wake Bertha
Sospeter amesema wazee hawathaminiwi
pale wanapokwenda katika vituo vinavyotoa huduma ya matibabu hali
inayowakatisha tamaa na kuitaka serikali kutambua kuwa wazee wananchango mkubwa
katika maendeleo ya Nchi.
Naye mzee Dionizi Kyaruzi
Rwabwigamo ameimba serikali kujenga vituo vya Afya na zahanati za serikali
katika kijiji chao hili kusogeza huduma ya Afya karibu ambapo itawaepushia
ghama wanazotumia kufuata matibabu katika umbali mrefu.
Mwenyekiti wa Kijiji cha
Rwambaizi Gosbert Paulo Katabarwa amekiri kuwepo changamoto ya ukosefu wa
Zahanati na Kituo cha Afya katika kijiji hicho na kuwa hali hiyo inasababisha
wazee wengi katika kijiji hicho kupata matibabu kwa shida japo hana idadi
sahihi ya wazee walio katika kijiji chake.
Post a Comment