Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WAHIMA MKOANI KAGERA WAOMBWA KUTAMBULIWA KUWA NI WATANZANIA HALALI WASIBAGULIWE.
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Jamii   ya   wahima   mkoani   Kagera   wametoa wito kwa   mamlaka   za   serikali   zinazohusika    na   usimamizi   wa   ...







Jamii  ya  wahima  mkoani  Kagera  wametoa wito kwa  mamlaka  za  serikali  zinazohusika   na  usimamizi  wa  utambuzi  wa    uraia  kuacha  kutumia  kigezo  cha  sura  ya  mtu  au  umbile  lake  kama  kigezo cha  kusema  siyo  Mtanzania.

Wametoa  wito  huo   katika  mkutano  mkuu  wa  kupitisha  katiba  ya  chama  cha  Wahima  ambao  ni  wanyambo  jamii  ya  wafugaji  wanaopatikana  maeneo  mbalimbali  ya  mkoa  wa  Kagera  kutokana  na  shughuli  yao  ya  ufugaji  kuhama  hama,wamesema  historia  yao  inaonesha  walikuwepo  hata  kabla  ya  uhuru  hivyo wanaomba  manyanyaso  na  usumbufu  wanaoupata  kutoka  kwa  mamlaka  hizo   kutambua  sura  siyo  kigezo  cha  kumtenga  mtu  kuwa  siyo  Mtanzania.

Wamesema  kuwa  wamekuwa  wakinyanyaswa  kila  mara  na  tayari  wameishafanya  jitihada  kadhaa  za  kuieleza  serikali  kuwa   jamii  ya  wahima  ni  wanyambo  wanaopatikana  mkoani  Kagera  hivyo wana  haki  zote  kwani  wao  ni  Watanzania  wazawa.

Mwalimu Samueli  Rwehindi  akisoma  rasimu  ya  Katiba  ya  umoja  huo  ambayo  imefanyiwa  marekebisho  ya  mwisho  na  kupitishwa  na  wajumbe  wa  mkutano  mkuu  ambao  ni  wanachama  alikuwa  na  haya  ya  kubainisha.

Aidha wajumbe  hao  waliweza  kuchangia  pesa  za  kuhakikisha  siku  ya  utamaduni  wa  mnyambo  ambayo  huadhimishwa  kila  ifikapo  tarehe  21  mwezi  wa  tano kila  mwaka  wamesema  siku  hiyo  wataonesha  kuwa  wao  ni  wanyambo  asilia  kwa  kuonesha  bidhaa  mbalimbali  za  utamaduni  wa  Mnyambo.

Hata  hivyo mwenyekiti  wa  WAHIMA  LUSHANDAGO PAULO  BWANAKUNU amewataka  wanachama  hao  kutilia  mkazo  elimu  kwa  kupeleka  watoto  wao  shule  ili  waweze kujikomboa  kutoka  na  manyanyaso  wanayoyapata  kwa  sasa  ambayo  yanachangiwa  na  kukosa  elimu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top