Wananchi wametakiwa kupanda
mazao ya chakula yanayokomaa kwa muda mfupi ili kujikinga na njaa ambayo
inaweza kusababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Rai hiyo imetolewa leo na
mwenyekiti wa kijiji cha Amulama kata ya Kamagambo wilayani Karagwe Jackson
Bitungwaramile wakati akiongea na Karagwe Forum
Jackson amesema kutokana na
mabadiliko ya tabia ya nchi kila mwanajamii anatakiwa kupanda mazao
yanayovumilia ukame na kusitawi kwa muda mfupi katika kujiwekea taadhali ya
chakula hapo baadae.
Amesema kwa yeyote atakayeshindwa kufanya
hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake maana wanaweza kusababisha
Kaya nyingi kukosa chakula.
Hata hivyo
Mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya ya
Karagwe wiki hii
alitoa kauli kuwa
kila Kaya kuwa
na hekali moja
ya viazi vitamu
na tayari watendaji
wa kata wameishaagizwa kusimamia
hilo na Kaya
itakayoshindwa kufanya hivyo
hatua kali za
kisheria zitachukuliwa.
Post a Comment