Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WAFANYABIASHARA SOKO LA KAYANGA WAOMBA UVUMILIVU KUPATA ENEO JINGINE LA SHUGHULI YAO
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wafanyabiashara   wa   soko   la   Kayanga   waliokumbwa   na   janga   la   kupoteza   bidhaa   zao kwa kuteketea   kwa bi...







Wafanyabiashara  wa  soko  la  Kayanga  waliokumbwa  na  janga  la  kupoteza  bidhaa  zao kwa kuteketea  kwa bidhaa hizo  zenye  thamani  ya  shilingi  zaidi  ya  billion  moja  wameombwa  kuwa  watulivu  na  wavumilifu  wakati  serikali  ikitafuta  ufumbuzi  wa  haraka  wa  kutatua  changamoto  inayowakabili  ya  sehemu  ya  kufanyia  shughuli  zao  lakini  pia  kwa  wale  ambao  walikuwa  na  mikopo  ya  taasisi  za  fedha.



Wito  huo  umetolewa  leo na  Mbunge  wa  Jimbo  la  Karagwe  Innocent  Bashungwa  wakati akiongea  na  wananchi  na  wafanyabiashara  hao  katika  mkutano  wa  hadhara  uliofanyika  eneo  la  soko  hilo  la  Kayanga  kwa  ajili  ya  kuwapa  pole  waathirika  hao  wa  janga  la  moto  pia  kuwaeleza  jitihada  alizochukua  katika  kuhakikisha  changamoto  hiyo  inatatuliwa  haraka  iwezekanavyo.



Amesema  kuwa anatambua  kuwa   hasara  na  uchungu  walionao  wafanyabiashara  hao  na  wananchi  kwa  ujumla  kutokana  na  janga  hilo  lakini  akawahakikishia  kuwa  yeye  kama  mwakilishi  atapambana  kuhakikisha  ufumbuzi  unapatikana  haraka  na  shughuli  za  biashara  zinaendelea  ili  watu  waendelee  kutafuta  riziki  yao  ya  kila  siku.

Bashungwa  amesema  suala  la  zimamoto  kutoza  ushuru  wakati  hakuna  huduma  inayotolewa  atahakikisha  analifuatilia  kwa  karibu  na  kuhaidi  atahakikisha  kwenye bunge    analiwasilisha  na  haswa  ikifikia  bajeti  ya  wizara  ya  mambo  ya  ndani  atahakikisha  anapewa  majibu  ya  uhakika.







Aidha   amesema  kuwa  miundo  mbinu  ya  soko  hilo  inabidi  kuiangalia  kwa  upya  wakati  wakijenga  soko  hilo  upya  ili  likitokea  tatizo  huduma  za  uokoaji  ziweze  kuwa  rahisi  kusaidia  kuokoa.




Hata  hivyo  Mbunge  wa  Jimbo  la  Karagwe  Innocent  Bashungwa  amesema  kuwa   atakaa  na  taasisi  za  fedha  zilizokuwa  zimetoa  mikopo  kwa  wafanyabiashara  hao  kuona  ni  njia  ngani  za  kuwasaidia  kwa  kipindi  hiki  ambapo  hawafanyi  kazi  zao.




About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top