Maelezo
ya mwanzo ya Tunda Man amesema ‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show
yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10
alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe
kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga
tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari
imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki.
Tunda
Man anamalizia kwa kusema ‘Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na
Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu
yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya
tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu
aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo
Post a Comment