TAARIFA KWA UMMA
MABADILIKO YA URUSHAJI WA MATANGAZO YA RADIO NA
TELEVISHENI WAKATI WA VIKAO VYA BUNGE
___________
1.0. UTANGULIZI
Ili kuhakikisha kuwa Matangazo ya Bunge yanaendelea
kurushwa na Televisheni nyingi hapa Nchini. Ofisi ya Bunge imeamua kuboresha
mfumo wa urushaji wa Matangazo ya Bunge kwa Bunge lenyewe kurusha Matangazo ya
Vikao vyake pamoja na Vipindi mbalimbali vyenye Maudhui kuhusu Shughuli za
Bunge ambazo hazijapata fursa ya kufahamika vyema kwa umma kuanzia katika
Mkutano ujao wa Bunge la Bajeti unaoanza tarehe 19 Aprili, 2016.
Huu ni Utamaduni wa kawaida kwa kila Bunge hususani
Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kuwa na Studio yake kwa lengo la
kurusha Matangazo ili yawafikie wadau kwa lengo la kurusha kupitia vituo vyao.
Jukumu la kurusha Matangzo ya Vikao vya Bunge
litafanywa na Bunge lenyewe kupitia FEED MAALUM ili kurahisisha kila Kituo cha
Radio na Televisheni kupata Matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga
Mitambo yao Bungeni Dodoma.
2.0 UTARATIBU MPYA WA URUSHAJI MATANGAZO
Ili kuhakikisha kuwa vituo vya Redio na Televisheni
vinapata matangazo ya Bunge, kila kituo cha Televisheni na Redio kitatumia
Masafa ya Matangazo ya Bunge (Frequencies) bure kupitia FEED MAALUM
itakayorushwa na Satellite ya INTELSAT 17 ambayo iko nyuzi 66 Mashariki kwa
masafa yafuatayo:
3.0 HITIMISHO
Mabadiliko haya hayataathiri usajili wa Waandishi wa
Habari wengine kuja Bungeni kwa ajili ya kufanya Coverage ya Shughuli za Bunge
ambazo hazihusishi kuingiza kamera ndani ya ukumbi wa Bunge. Utaratibu huu
mpya, utakuwa umesaidia kuondoa hali ya kila Kituo cha Televisheni kufunga
Mfumo wake wa Kurusha Matangazo kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma na
badalayake yatapokelewa katika Vituo vya Televisheni na Redio kupitia Masafa
tajwa hapo juu. Utaratibu huu ni wa kawaida katika
Mabunge takribani yote Duniani husani wanachama wa
Jumuiya ya Madola.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM.
15 Aprili, 2016.
Post a Comment