Wilaya ya
Kyerwa mkoani Kagera imeendelea
kukumbwa na janga
la maafa kutokana
na mvua za
msimu wa masika
kunyesha huku zikiambatana na
upepo mkali kuangusha
migomba na kuezua
nyumba za wananchi
katika maeneo kadhaa
ya wilaya hiyo.
Mvua iliyonyesha jana
katika kijiji cha
Nshunga kata ya
Kyerwa imekuwa mwendelezo
wa maafa huku pia
ikisababisha maafa kama
hayo kwenye kijiji cha
Ruhita kata ya
Kamuli.
Wenyeviti wa
vijiji hivyo wakiongea
kwa nyakati tofauti
wamesema kutokana na
maafa hayo wananchi
wa maeneo yao
hawana budi kulima
mazao yanayostawi kwa
muda mfupi ili
kujikinga na janga
la njaa kwani
wengi wao hutegemea
migomba kupata zao la ndizi ambalo
ni chakula chao
kikuu.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha
Ruhita kata ya Kamuli Wilayani Kyerwa
Salvatory Baziwani , akizungumza na chombo hiki kwa njia ya simu mapema leo ,amesema mvua iliyonyesha jana kwa
kuambatana na upepo na mawe,imeezua baadhi ya nyumba na kuharibu migomba na kuwaacha wakazi hao katika hali ya
wasiwasi namna watakavyopata chakula.
Wananchi wa Ruhita kata kamuli
wameeleza masikitiko yao juu ya mvua hizo,kwani wakati inaanza kunyesha
ilionyesha haina upepo mkali na badaye iliongezeka kwa kuambata na mawe makubwa
ambapo wameiomba serikali kuangalia msaada unaowezekana hususani chakula hata
kama sio wakati huu lakini kuwaweka katika mpango wa namna gani watakavyojikimu
kwa mda mfupi ujao.
Naye
Mwenyekiti wa serikali
ya kijiji cha Nshunga kata
Kyerwa Gerad Colonery amesema kuwa
Idada ya Nyumba zilizoezuliwa na
upepo na mazao kuharibiwa kufuataia Mvua
kubwa iliyonyesha jana majira ya saa 9 alasiri
ikiambatana na upepo mkali na mawe
imezidi kuongezeka baada ya kubainika vitongoji vingine 2 vilivyokubwa
na maafa hayo katika kijiji cha hicho.
Ametaja
vitongoji vilivyoongozeka
kuwa ni Nshunga na Songa Mbele ambapo
vilivyoripotiwa awali vilikuwa
Viwili Kitongoji cha Nyakagera na
Omukishanda Stesheni hivyo kufanya
idadai ya vitongoji 4 vilivyokumbwa na maafa hayo kati vitongoji 6 vinavyounda
kijiji hicho.
Mwenyekiti
huyo amethibitisha kuwepo majeruhi wawili ambao ni watoto walioangukiwa na
Tofali za Nyumba japo hawakupata majeraha makubwa.
Amesema usalama
wa wananchi na mali zao umeelezwa kuimarika kwa
kuwa kijiji kimejipanga
kuepuka wizi au
udokozi wowote ule
katika kipindi hiki.
Mwenyekiti wa
kijiji cha Nshunga
kata ya Kyerwa
amesema kwenye kijiji
chake kamati ya
maafa ya kata
inaendelea na tathimini na
majibu rasmi yatatolewa
kesho na kuongeza
kuwa mikakati iliyopo wakati
wananchi wakisubilia hatua
nyingine amsema amejipanga kuitisha mkutano
wa Alhamisi wiki
hii kuweka mpango.
Hata
hivyo maafa kwa
kipindi cha kuanzia
machi 29 mwaka huu yameripotiwa kutokea
katika maeneo kadhaa
ya wilaya ya
Kyerwa kwenye kijiji cha
Kigorogoro kata ya Kibale.
Post a Comment