Vibanda vilivyoteketea kwa
moto kwenye soko
la Kayanga wilayani
Karagwe Mkoa wa Kagera
ni 117 kati ya
vibanda 247 ambapo thamani yake
halisi haifahamika kwani timu
ya wataalamu inaendelea na
zoezi la tathimini ya hasara iliyotokea.
Akizungumza na
waandishi wa habari
jana ofisini kwa
Mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya ya
Karagwe Walles Mashanda alisema
soko kuu la
Kayanga lilikuwa na
vibanda vya aina
mbili la kwanza
vile ambavyo vinazunguka
soko kwa nje
ambavyo jumla yake
ni 112 na vilivyo
ungua ni 34 na
mpangaji alikuwa akilipa shilingi 25000 kwa
mwezi hivyo hasara
yake kwa vilivyoungua
ni shilling 850,000 kama ushuru
wa halmashauri.
Alisema aina
ya pili ni
vibanda vya ndani
ya soko ambavyo
vilikuwa vimejengwa kwa
mbao jumla yake
ni 135 na vilivyoungua
ni vibanda 83
ambavyo ushuru wake kwa
mwezi ilikuwa shilingi
10,000 ambapo jumla yake
ni shilling 830,000 kwa
mwezi hivyo halmashauri
imepata hasara ya
kukosa ushuru kwa
mwezi huu kwa
shilingi 1,680,000 kwa
vibanda vyote 117 vilivyoungua.
Mashanda alisema
hizo ni hesabu
za haraka lakini
bado timu ya
watalaamu ya halmashauri
pamoja na serikali
kuu kwa kushirikiana
na kamati ya
ulinzi na usalama
inaendelea na zoezi
la kutathimini hasara
halisi iliyotokana na
moto huo na
kuomba wananchi haswa
wafanyabiashara waendelee kuvuta
subira kwani kila
hatua serikali na
mamlaka husika zitawataarifu.
Alitaja baadhi
ya mikakati ya
halmashauri ya haraka
waliojadiliana kwa leo
katika kikao kuwa
ni pamoja na kukusanya takataka
zilizopo kwenye soko
hilo kwani kuna
baadhi ya watu
hawana elimu ya
athari za uchafu
kwani walikuwa wakiokota
vitu hata watoto
kuokota pipi kwenye
uchafu huo.
“Unajua kwenye eneo
letu hili kuna
baadhi uelewa wa
masuala ya majanga
na athari najua
hawana pale kuna
mafuta,nguo vitu vya
plastiki viliungua vinatengeneza
kemicals sasa watoto
wanaokota pipi wengine
hata wanadiriki kutoa
hata sukari iliyoungua
hiyo ni hatari”Alisema Mashanda.
Mashanda alisema
mikakati mingine ni
kubomoa majengo yaliyoharibiwa na
moto hivyo kujenga
upya na kwa
kubadili miundo mbinu
kwani ilyopo ni
ya zamani hivyo
kutakuwepo milango mikubwa
ya kuruhusu hata
magari ya zima moto
kuingia pindi tatizo
linapojitokeza.
Aliwataka wafanyabiashara na
wananchi kwa ujumla
kujenga tabia ya
kujiunga na Bima
ili linapotokea majanga
kama kunguliwa nyumba
au athari nyingine
iwe rahisi kupata
usaidizi wa haraka
kuliko ilivyo sasa.
Mashanda alielezea
kusikitishwa kwake na
vitendo vya baadhi
ya watu wasio wema
badala ya kuokoa
wao waligeuka wavamizi
na wezi wa
msali za waathirika
wa moto huo na kuongeza
kitendo hicho hakivumiliki
na siyo cha
kiungwana kumtendea mtu.
Mkuu wa
wilaya ya Karagwe
Deodatus Kinawiro ambaye
pia ni mwenyekiti
wa kamati ya
ulinzi na usalama
amepiga marufuku kwa
mtu yeyote kuokota
kitu chochote kwenye
eneo la soko
lilipoungua na atakaye
kiuka agizo hilo hatua
kali zitachukuliwa dhidi
yake.
Alisema ulinzi
utaendelea kuimarishwa kwenye
eneo hilo kwani
kuna baadhi ya
mali za wafanyabiashara ambazo
wakati wa kuokoa
kuna vibaka na wadokozi waliiba
mali hizo.
Hata hivyo
mkuu wa kikosi
cha zimamoto wilaya
ya Karagwe Peter
Mbale alisema kuwa
malalamiko ya wananchi kuhusu
ushuru wa zima moto
wanaotoa ni kuwa
upo kisheria na
nitozo ya serikali
lakini akaongeza kuwa
jitihada zinaendelea kufanyika
kuona kama gari
litapatikana la kuzima
moto pindi janga
kama hili litajitokeza.
Alisema kutokana
na baadhi ya wafanyabiashara kutozingatia ushauri
wa jeshi la
zimamoto kwani wengi
walipuuza zuio la
kutopikia sokoni humo
na kutouza mkaa
lani watu walipuuza.
Alisema ndiyo
maana hata jana
hakukwa na tatizo
lolote magari ya
zimamoto yaliruhusiwa mara
moja wakati walipowasiliana kwani
tozo yao nayo
ilichangia kupata magari
hayo kwa haraka
sana.
Post a Comment