Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA NNE YAMETANGAZWA RASMI NA NECTA.
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wa...
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.

Akitangaza matokeo hayo jana  Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango cha ufaulu.

Jumla ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87 waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C,na D. Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu usioridhisha.

Aidha wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Sayansi kwa asilimia 89.44, na baraza limewataka walimu kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi waliofanya vibaya ili wawasaidie kuimarika na waweze kupata ufaulu mzuri.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top