Zamani
wakati tupo shule ya msingi tulikua na utamaduni wa kushindana eti nani ana
mwandiko mzuri😄. Yaani, zoezi hilo lilionekana la maana
kuliko kusoma. Kuna baadhi yetu tuliobahatika kuwa na miandiko isiyopendwa,
tukawa tunahangaika kubadilisha kalamu ili tuandike vizuri. Yaani, tunaamini
ukiwa na kalamu fulani basi utakua na mwandiko mzuri.
Sasa
cha kujiuliza, mbona fulani yeye hasumbuki na kalamu na mwandiko wake ni mzuri
tu. Yaani yeye ukimpa Bic, Cello au nyingine yoyote, ataandika vizuri tu
Maisha
ni kama muandiko. Unajikuta unajishughulisha na kulaumu mazingira
yanayokuzunguka kama sababu za kushindwa au kufanikiwa. Yaani unajisemesha
👉🏿
"mie ningesoma mie, nisingekua hapa"
👉🏿mie
ningekua mtoto wa bakhresa, ningeisha jenga ghorofa
👉🏿ningezaliwa
ulaya mie, nisingekua hivi
👉🏿ningekua
na mtaji mkubwa, ningeishatoka
Yaani,
hufikirii kama WEWE ni tatizo. Unaamini kabisa mazingira uliyopo ndio chanzo
cha kushindwa kwako. Unaiambia akili yako kila siku kuwa tatizo ni mazingira na
sio WEWE.
Usichojua
(au usichotaka kuamini) ni kwamba,
👉🏿kuna
watu wamesoma na wana mafanikio kidogo
👉🏿Kuna
watu wamezaliwa Ulaya na hata hawasomeki.
👉🏿kuna
watu wamezaliwa na wazazi matajiri na hata hawana lolote la kujivunia
👉��kuna
watu wamekua na mitaji mikubwa na hawajafika popote.
Maisha
haya yanajengwa na imani uliyo nayo. Yanaongozwa na kile kilichopo katika
kichwa chako. maisha unayoishi leo ni
matokeo ya mawazo yako ya jana. Sasa maisha yako ya kesho ni matokeo ya mawazo
yako ya leo.
👉🏿Unajiambia
nini mwenyewe?
👉🏿Unaamini
kipi kutoka katika kile unachoambiwa na wenzio?
👉🏿Unaruhusu
mawazo gani yakutawale? Hasi au chanya?
Haya
yote yanamtengeneza mtu uliyepo sasa. Kile unachojiambia mara kwa mara hata
kama sio kweli ndicho akili yako inakitengeneza na kuruhusu utende kama imani
yako ilivojijenga.
Ukijiambia
huwezi hesabu. Yaani wewe kila mara unajisemesha tu "mie hesabu
siwezi" basi akili yako itaamini na hivyo utatenda kama akili yako
inavyokutuma. Utajikuta husomi vitabu vya hesabu...kwa kuwa ukisoma utafaulu na
hiyo ni kinyume na imani yako.
Utajikuta
huendi kwenye discussions za hesabu kwa kua ukienda, utafaulu na hiyo ni
kinyume na imani yako.
Vivyo
hivyo katika biashara na kazi. Ukijiambia mara kwa mara kuwa "mimi hii
kazi siwezi" "mie biashara siwezi kabisa hii", hicho ndicho
kitakachotokea.
Napoleon
Hill anasema "whatever the mind of man can conceive and believe, it can
achieve.." yaani, chochote kile ambacho akili ya binadamu inajazwa kwacho
na inaamini basi itafanikiwa kukipata.
👉🏿Jaza
akili yako na mawazo ya kukujenga.
👉🏿Soma,
sikiliza na angalia mambo yanayokupa nguvu na sio ya kukutisha na kukukatisha
tamaa.
👉🏿wapotezee
marafiki vimeo ambao kila kukicha stori zao ni jinsi ilivyo ngumu kufanikiwa
katika jambo fulani iwe , kazi, biashara
au mahusiano.
Mwandiko
wako unaweza kuuweka vizuri pasipo kutegemea na ni kalamu gani unatumia katika
kuandika.
Maisha
ni mwandishi na sio kalamu📝
Post a Comment