Mbunge
wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema yupo tayari kulipa kodi
ya mapato ya Sh586 milioni iwapo Mahakama itaamuru hivyo.
Kodi
hiyo inatokana na Sh1.617 bilioni alizopewa
na mfanyabiashara maarufu nchini, James Rugemalira ambazo zilidaiwa kuchotwa katika akaunti ya
Tegeta Escrow.
Profesa
Tibaijuka aliyasema hayo jana baada ya taarifa kwamba Bodi ya Rufani ya Kodi
Tanzania (TRAB), imeagiza utekelezaji wa suala hilo ili kutimiza matakwa ya
sheria kuhusu mapato nchini.
“Ni
kweli ninadaiwa kodi ya Sh586 milioni, ila nimeenda mahakamani kutaka ufafanuzi
kama ni halali kufanya hivyo kwa fedha zilizotokana na mchango,” alisema
Profesa Tibaijuka na kuongeza “Nilipewa fedha kwa ajili ya shule lakini nadaiwa
kama ni kipato binafsi, hivyo nataka Mahakama iseme, ikikubali nitalipa bila
shida yoyote.”
Mbunge
huyo alifafanua kuwa, anatambua kulipa kodi ni suala la kila mwananchi na
anachotaka ni ufafanuzi wa uhusiano uliopo kati ya mapato na kodi.
Alisema
lengo ni kutaka kujua iwapo mchango ni sehemu ya fedha zinazostahili kutozwa
kodi, bila kujali zimepokelewa zikiwa taslimu au kupitia kwenye akaunti benki.
“Nipo
msibani hivi sasa. Watu wanakuja kunipa pole, wengine wanatoka Dar na wasioweza
wanatuma michango yao na hapa ndipo nisipoelewa dhana ya kodi kwenye michango.
Hii nayo inastahili kuingizwa kwenye mkumbo huo?” alihoji.
Msemaji
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo alithibitisha kutolewa kwa
hukumu hiyo kwenye pingamizi la makadirio aliloliweka mbunge huyo na kueleza
kuwa bado anaweza akatafuta haki kwenye mamlaka za juu kama hajaridhika.
“Shauri
lake liliamriwa Machi 29 na akatakiwa kulipa kiwango hicho alichokadiriwa,”
alisema.
Mbunge
huyo wa Muleba Kusini, alitakiwa kulipa fedha hizo baada ya TRAB kutupilia
mbali rufaa yake ya kupinga kulipa zaidi ya Sh500 milioni.
Profesa
Tibaijuka, Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikata
rufaa hiyo baada ya TRA kumtaka alipe kodi ya mapato Sh586,364,625 kutokana na
fedha alizopokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering and
Marketing Limited, Rugemalira.
Profesa
Tibaijuka ambaye alipokea fedha hizo kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya
Mkombozi, zilisababisha kuvuliwa uwaziri na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
Alisema
fedha hizo hazikuwa zake binafsi bali zilitolewa msaada kwa Taasisi ya Joha
Trust.
Hata
hivyo, TRA kupitia kwa Wakili wake, Noah Tito ilisema Tibaijuka anawajibika
kulipa kodi hiyo kwani fedha hizo ziliingia katika akaunti yake
Post a Comment