Jumla ya miradi kumi ya
maendeleo ya wilayani Karagwe mkoani Kagera yenye thamani ya shilling milioni
911,695,000 e inatarajiwa kuzinduliwa na kuwekea jiwe la msingi wakati
wa mbio za mwenge wa uhuru ambao
utapokelewa wilayani Karagwe tarehe 26 mwezi wa 7 mwaka huu
Hayo yamesemwa leo na
mratibu wa mbio za mwenge wilaya ya Karagwe Aloyce Mjungu wakati akiongea na
waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mbio za mwenge ambayo yanaendelea
katika wilaya hii.
Mjungu amesema kuwa mwenge
wa uhuru utapokelewa tarehe 26 mwezi wa saba mwaka huu katika shule ya msingi
Muungano katani Nyakasimbi na ndiko utaanzia kutembelea miradi ya maendeleo
ambapo utaweka jiwe la msingi katika nyumba ya walimu yenye vyumba sita shule
ya Sekondari Nyakasimbi yenye Thamani ya shilingi milioni 150.
Ametaja miradi mingine kuwa
ni uzinduzi wa club ya wapinga Rushwa katika shule ya sekondari Rugu,uzinduzi
wa shamba la miti Kasheshe Rugu pamoja na miradi mingine kama anavyoeleza.
Ameongeza kuwa baada ya uzinduzi wa miradi
hiyo yote mwenge utakesha katika viwanja vya Changarawe mji mdogo wa Kayanga na
wataukabidhi wilayani Kyerwa tarehe 27 mwezi wa saba mwaka huu katika shule ya
msingi Ilega iliyoko katika kata ya Mabira wilayani Kyerwa.
Mjungu amewataka wananchi
kuchangia mwenge wa uhuru kwani unakuja kwa ajili ya wananchi wote bila kujali
kabila,rangi au itikadi.
Post a Comment