WATUMISHI HEWA MKOANI SHINYANGA WAFIKIA 226 KUTOKA ZERO ILIYOKUWA IMETAJWA
Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK John Pombe Magufuli wakati akizindua rasmi daraja la Kigamboni.
Amesema taarifa alizonazo mpaka sasa ni kuwa watumishi hewa katika mkoa huo wa Shinyanga wamefikia 226 kutoka ZERO iliyokuwa imewasilishwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango ambaye alitimuliwa kazi baada ya kubainika aliidanganya IKULU.
Rais Magufuli amesema ni lazima kuwajibika kwa watanzania wanyonge ili nao waweze kunufaika na matunda ya nchi hii.
Aidha Rais Magufuli amekataa Daraja la Kigamboni kuitwa jina lake na badala yake amependekeza liitwe jina la muasisi wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwani mawazo ya kujenga daraja hilo yaslianza wakati wa kipindi cha utawala wa mwalimu Nyerere.
Post a Comment