Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KASI YA RAIS MAGUFULI NI NGUMU KUTETELEKA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ATUMBULIWA LEO.
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Rais Magufuli amemsimamisha kazi leo     Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe kutokana na ufisadi wa kutisha katika...





Rais Magufuli amemsimamisha kazi leo   Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe kutokana na ufisadi wa kutisha katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji  na  kuisababishia  serikali  hasara  ya  sh. bilioni 3.







Rais Magufuli amechukua uamuzi huo leo  wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda ametoa Hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top