RAIS
John Magufuli amezua mjadala baada ya kuvamia tawi la CRDB (Holland Branch),
akiwa kwenye gari namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya "Adamu na
Hawa" wala bendera ya Rais.
Tukio
hilo lililochukuwa dakika 25, limetokea majira ya asubuhi jijijni Dar es Salaam
katika tawi hilo ambalo liko katika makutano ya barabara za Ohio na Samora,
bila kutarajiwa.
Mara
baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo, makutano ya
barabara hizo yalifungwa ndipo Rais aliposhuka kwenye gari na kuingia ndani ya
benki hiyo.
Wakati
akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa wakijiandaa
kuingia ndani ya benki hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale
ambao waliyokwishaingia.
Aidha,
baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine
walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa
sitaili ile. Baadhi ya wananchi walisema hawajaona tukio kama lile kwa Marais
wote waliyopita.
James
Charles, ambaye ni dereva wa taxi, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye
eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimarishwa walishituka na mara wakamuona Rais
Magufuli akishuka kwenye gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea
ofisi yake ya zamani.
“Lakini
kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB, tukajiuliza vipi
rais leo kaamua kuwa kama mteja? Hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa
inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu. Haiwezekani aende akachukue fedha
kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,”alisema Charles.
Joyce
Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema kuja
kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda
pale kwa ajili ya kutumbua majipu.
“Mimi
wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma.
Kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,” alisema.
Baada
ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari
huku akiwapungia mkono wananchi.
Post a Comment