Tasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa TAKUKURU mkoani KAGERA imepokea jumla ya malalamiko 363 na kufungua kesi
21 mahakamani ikiwa kesi zinazoendelea mpaka sasa ni 34 kuanzia kipindi cha
julai 2015 hadi machi 2016.
Akizungumza na vyombo vya habari
mkuu wa Taasisi hiyo mkoa wa Kagera JOSEPH
MWAISELO amesema kuwa majalada yaliyokamilika kuchunguzwa ni 34 kesi
zilizoshindwa na tasisi hiyo 17 na kesi ambazo ziliwashinda tasisi hiyo ni 10.
Akitoa mchanganua wa kesi
hizo,MWAISELO amesema kuwa kesi nyingi zinatoka katika idara mbalimbali ikiwemo
maeneo ya vijiji na mitaa halmashauri na sekita binafsi.
Amebainisha kuwa ili kutoa elimu ya
kutosha kupinga vitendo vya upokeaji rushwa tayari club mbali za wanafunzi
mashuleni na vyuoni za kudumu zimeundwa ili wanafunzi hao wanapohitimu
waendelee kuelimisha uma kuhusiana na vitendo hivyo.
Mkuu huyo akatumia fursa kuainisha mikakati
ambayo imeweka na tasisi hiyo lengo kubwa ikiwa ni kuisaidia serikali kukusanya
mapato.
Post a Comment