Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani Mbunge wa Jimbo la Ubungo Sued Kubenea
kwa kosa la kutoa lugha chafu ya matusi kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mbunge
huyo amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu nje kwa masharti ya kutorudia kosa la
namna hiyo katika kipindi hicho na endapo atarudia kosa hilo basi atakuwa
amevunja masharti ya kifungo hicho na kustahili kifungo cha gerezani.
Akitoa
hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema baada ya kupitia ushahidi
na vielelezo vilivyotolewa mahakamani hapo mtuhumiwa amepatikana na hatia baada
ya upande wa mashtaka kuthibitisha bila chembe ya wasiwasi kuwa mtuhumiwa
alitenda kosa hilo.
Hukumu
hiyo imefuatia ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu kwa upande wa mashtaka
wakiongozwa na Mheshimiwa Makonda huku upande wa utetezi ukiwa na mashahidi
watatu akiwemo Kubenea mwenyewe.
Saed
Kubenea alikuwa anakabiliwa na shtaka la kutoa lugha chafu kwa Makonda wakati
wakiwa katika Kiwanda cha Ushonaji na Usafirishaji wa nguo cha Tooku Garments
Co. Ltd kilichopo maeneo ya Mabibo External baada ya kutokea kutokuelewana
baina ya viongozi hao walipokwenda kutatua mgogoro wa wafanyakazi wa kiwanda
hicho na wamiliki.
Katika
kesi hiyo, Kubenea anadaiwa kumtolea lugha chafu Makonda kuwa ‘wewe kibaka,
mpumbavu, mjinga na cheo chenyewe cha kupewa tu’.Upande wa mashtaka ulikiri
kutokuwa na rekodi yoyote mbaya ya mtuhumiwa huyo na kwamba hili ni kosa lake
la kwanza lakini wakaiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu
wengine.
Awali,
akijitetea baada ya kutiwa hatiani Kubenea alisema, hakwenda pale kwa nia mbaya
ya kutukana bali alikwenda kutatua mgogoro uliokuwepo baina ya wafanyakazi na
wamiliki wa kiwanda hicho na kwamba hakuwa na miadi yoyote na aliyekuwa Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ya kukutana pale.
Akijitetea
zaidi Kubenea aliiomba mahakama impatie adhabu nafuu kwakuwa yeye ni Mbunge wa
Jimbo la Ubungo ameajiriwa kuwatumikia wananchi.
Post a Comment