Vilabu
vya Geita Gold FC, Kanembwa JKT na JKT Oljoro vimeshushwa daraja kutoka ligi
daraja la kwanza hadi ligi daraja la pili kwa kosa la kupanga matokeo katika
mechi zao za Mwisho.
Baaada
ya timu hiyo kushushwa daraja timu ya Mbao FC ya Jijini Mwanza imepanda daraja
hadi ligi kuu.
Hukumu
hiyo Imetolewa Jumapili hii na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu ya TFF
Wakili Jerome Msemwa.
Katika
hukumu hiyo inayohusu kesi ya kupanga matokeo ya mechi za Kundi C za ligi
daraja la kwanza, Mwenyekiti wa Chama
cha soka mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo nae amekutwa na hatia hiyo hivyo
kufungiwa maisha kutojihusisha na soka katika maisha yake yote.
Wengine
waliokumbwa na makosa ya kupanga matokeo ni mlinda mlango Denis Richard wa
Geita Gold na mlinda mlango wa Kanembwa Mohamed ambao wamehukumiwa kifungo cha
miaka 10 na faini ya Shilingi milioni 10.
Kocha msaidizi wa Geita Choki Abeid
nae amefungiwa maisha kujihusisha na soka.
Fateh Remtullah katibu Mkuu Polisi
Tabora nae kafungiwa maisha kwa kosa la kupanga matokeo kwa kumshawishi mwamuzi
asimalize mpira.
Benard Fabia kocha msaidizi Polisi
Tabora amefungiwa maisha kujihusisha na soka kwa kosa la kupanga matokeo kwa
kuwazuia wachezaji wake wachelewe kutoka katika vyumba vya kubadilishia nguo.
Saleha Mkelemi mwamuzi Polisi Tabora
na JKT Oljoro amefungiwa miaka kumi na faini ya milioni kumi, kwa kupanga
matokeo baada ya kuchezasha mpira kwa dakika 110 kipindi cha 53 - Kipindi cha
pili 57
Moshi Juma mwamuzi Geita Gold FC Vs
Kanembwa JKT nae amefungiwa maisha kujihusisha na soka kwa kosa la kupanga
matokeo kwa kuchezesha mpira kwa dakika 85 kipindi cha pili baadala ya dakika
45.
Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa
Geita Salum Kulunge hana hatia na
Constantine Morad Mwenyekiti wa timu ya Geita nae hana hatia.
Abbas Mtei katibu Mkuu wa Kanembwa
JKT hana hatia, Hussein Nalinga katibu Mkuu JKT Oljoro hana hatia, Alex Kataya
katibu Mkuu Polisi Tabora hana hatia.
Post a Comment