Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela juzi alivamia kituo cha Radio Ebony Fm
cha mjini Iringa na kuamuru kukamatwa kwa watangazaji wawili waliomuigiza sauti
yake, kuadhimisha siku ya wajinga duniani.
Kwa
siku kadhaa, Kasesela amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana
kusambaa kwa picha zinazomuonyesha akitekeleza majukumu yake.
Miongoni
mwa picha hizo ipo aliyokuwa akila mhindi, kubeba boksi la dawa, kuvusha watu
kwenye mafuriko na kulenga shabaha kwa kutumia bunduki aina ya SMG.
Watangazaji
waliokamatwa na baadaye kuachiwa ni Neema Msafiri na Edwin Dugange wanaotangaza
kipindi cha ‘Morning talk’
Post a Comment