Wananchi wanaomiliki Ardhi wametakiwa kufuata kanuni,
sheria na taratibu hasa katika kuziba na kuanzisha barabara ambazo zinapita
katika maeneo yao.
Wamesema hayo wananchi wa Mtaa wa Rwenjonjo eneo la
Ahakakoma Kata ya Ihanda katika mkutano
wa pamoja kufuatia kutaka kuzibwa kwa moja ya barabara iliyoko mkabala na
uwanja wa Ndege Ihanda kuelekea Kigasha.
Katika mkutano huo umehudhuriwa na wananchi wa maeneo
husika, viongozi mbali mbali akiwemo mwenyekiti wa mtaa huo, Diwani wa Kata ya
Ihanda na Afisa mtendaji wa Kata hiyo kwa agizo la Mkuu wa Wilaya ya Karagwe
kumaliza mgogoro wa moja ya barabara katika maeneo hayo kutaka kuzibwa na moja
ya familia ambao walipeleka mashtaka katika ofisi ya mkuu wa Wilaya kuwa
barabara hiyo imeanzishwa katika ardhi ya mtoto yatima.
Wanaolalamikia kuwepo kwa barabara hiyo hiyo ni Aquilina
Revelian na Eusebia Reveliana wanaodai kuwepo na barabara tatu katika ardhi yao
hivyo kutaka kuziba moja ya barabara hizo kwa lengo la kuokoa ardhi ya mtoto
yatima wanayemlea kwani ni eneo lake na kusema kuwa wanaotaka kuendeleza
barabara hiyo wanapaswa kukaa pamoja nao kwa ajili ya makubaliano na kupewa
fidia na si vinginevyo.
Aliyelalamikiwa na familia hiyo kwa kuanzisha barabara
hiyo ni Odilo Binemungu ambaye amesema
kuwa yeye hakwenda kuanzisha barabara mpya katika eneo linalodaiwa bali
alitimiza jukumu lake la kujitolea katika barabara hiyo kama ilivyo kawaida ya
wananchi wa eneo hilo na kusema kuwa barabara hiyo ameikuta tangu amezaliwa na
hana budi kuiendeleza.
Wazee wa eneo hilo walizaliwa kuanzia miaka ya 1930
wameeleza kuwa barabara hiyo ni ya tangu zamani na watu wa kuelekea Kigasha
walikuwa wanaitumia katika shughuli za maendeleo na haijaanzishwa leo wala jana
kama wafungua mashtaka wanavyosema.
Post a Comment