Afisa mtendaji wa kata ya Nyakasimbi wilayani Karagwe
mkoani Kagera Medard Baletwa amewaagiza viongozi wa vitongoji na vijiji kuhakikisha
wanasimamia zoezi la kilimo cha Kinga ya njaa kwa kila familia.
Baletwa amesema
kuwa ni bora wakulima wakatumia mvua
hizi zinazoendelea kunyesha kupanda mazao ya kinga ya njaa hususani yale
yanayokomaa kwa muda mfupi.
Amesema kuwa ni jukumu la kila kiongozi wa kitongoji na
kijiji pia kuhakikisha anasimamia kila familia inapanda mazao hayo ambayo ameyataja
kuwa ni mihogo,malando, viazi na magimbi ambapo kila familia itatakiwa kupanda hekali
kadhaa kama watakavyokuwa wameelekezwa.
Amesema kuwa kufuatia agizo la mwenyekiti wa Halmashauri
ya wilaya ya Karagwe Wailles Mashanda la afisa watendaji kusimamia kilimo cha
kinga ya njaa,Baletwa amesema atazungikia kata nzimakwa kushirikiana na
viongozi wa vijiji ili kuhimiza kilimo hicho pamoja na shuguli nyingine za
maendeleo.
Post a Comment