MKAZI
mmoja wa jijini Dar es salaam Husein Nahim (34 )amefikishwa katika mahakama
ya wilaya ya Karagwe MKOANI Kagera kwa tuhuma ya unyang’anyi wa kutumia
silaha na kupora kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 15 kwa mkazi wa kata
ya Kihanga wilayani Karagwe.
Akisoma
shitaka hilo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Paul Magoryo alisema kuwa,
mtuhumiwa alitenda kosa hilo februali 25 mwaka huu majira ya saa mbili
asubuhi wilayani humo.
Awali
upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi
Inspecta Stividana Webiro aliieleza Mahakama hiyo kwamba, mtuhumiwa siku ya
tukio alipita katika eneo la kata ya Kihanga wilayani Karagwe akiwa anaendesha
gari lenye namba za usajiri T 381 BWM aina ya Toyota Kalina pamoja na wenzake
wawili waliokuwa ndani ya gari hilo majira ya saa mbili asubuhi ambapo
mtuhumiwa alipofika eneo hilo alisimamishwa na mlalamikaji wa kesi hiyo Godwine
Kigo (22) mkazi wa kata hiyo ambaye alikuwa mkusanya ushuru na kumtaka
kumsafirisha ndani ya gari hilo hadi mjini Kayanga na wakakubaliana kuwa
alipe nauli kama abiria wengine kiasi cha shilingi 2,000.
Ilielezwa
mahakamani hapo kuwa mlalamikaji akiwa amepanda ndani ya gari hilo alipewa
sehemu mbele ya gari karibu na kiti cha dreva ambaye ni mtuhumiwa wa kesi
hiyo na kuulizwa na mtuhumiwa kuwa anaelekea sehemu gani ndipo mlalamikaji
alimjibu kuwa anaenda Kayanga benki ya NMB na hivyo amtelemshe maeneo hayo na
amlipe nauli mtuhumiwa.
Ilielezwa
kuwa, alipofika eneo hilo alidai kuwa anashida Katika maegesho ya magari
Kayanga na hivyo angemtelemsha hapo na ndipo alipitiliza hadi kanisa la
kathoric la Kayanga ambapo mlalamikaji aliombwa kupewa fedha hiyo aliyo
nayo kiasi cha shilingi 15.2 milioni kwa kutishiwa kupigwa risasi ndipo
alipotoa kiasi hicho kwa kuhofia usalama wake na mtuhumiwa pamoja na wenzake
wawili kutoroka na kutelekeza gari likiwa limepinduka kutoka umbali wa eneo la
tukio.
Aidha
mahakama ilieleza kwamba, mlalamikaji baada ya kunyanganywa fedha hizo alitoa
taarifa kituo cha polisi mjini Kayanga na jeshi la polisi lilimtia
mbaroni mtuhumiwa akiwa amejificha kichakani katika eneo la shule ya sekondari
Karagwe akiwa peke yake na akiwa ameisha badilisha nguo akijiandaa kukatiza
barabara huku akiwa hana fedha hizo ambapo aligunduliwa na wachunga ng’ombe .
Hata
hivyo upande wa mtuhumiwa alikana tuhuma hiyo inayomkabili na alirudishwa
rumande ambapo upande wa mahakama ulihairisha kesi hiyo kutokana na shauri hilo
kuendelea kusikilizwa mahakamani hapo.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Related Posts
- KAGERA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KUENDELEA KUJIIMARISHA KUWALINDA RAIA NA MALI ZAO25 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Vyombo ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya ...Read more »
- MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA WILAYA ZA KARAGWE NA NGARA PIA HITIMISHO WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mwenge wa Uhuru waendelea kuchanja mbuga Mkoani Kagera kwa ku...Read more »
- MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI KAGERA NA KUANZA UZINDUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YABILIONI 1216 Apr 20180
Na: Sylvester Rapahel Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na...Read more »
- TIMU YA WATAALAM WA UJENZI KUTOKA NCHINI CHINA YAKAGUA ENEO LA UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA ILI KUANZA UJENZI MARA MOJA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Serikali ya Watu wa China yatuma timu ya Wataalam wa Usanif...Read more »
- MKOA WA KAGERA WAVUKA LENGO KATIKA UNDIKISHAJI WA WANAFUNZI AWALI NA DARASA LA KWANZA MWAKA 201816 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mkoa wa Kagera wavuka lengo la uandikishaji wa Wananfunzi katika madarasa...Read more »
- MKUU WA MKOA KAGERA AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUFIKISHWA OFISINI KWAKE AKIWA NA PINGU MIKONONI BAADA YA KUITIA SERIKALI HASARA08 Mar 20180
Na Sylvester Raphael Mkuu wa Mkoa wa Kagera aagiza Mkandarasi wa Kampun...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.