Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WATANO WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UCHOMAJI KANISA KATOLIKI JIMBO LA KAYANGA KARAGWE
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
WAKAZI watano wa manispaa  Bukoba mkoani Kagera wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Karagwe kwa tuhuma ya kosa la uchomaj...





WAKAZI watano wa manispaa  Bukoba mkoani Kagera wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Karagwe kwa tuhuma ya kosa la uchomaji wa kanisa katoriki la kijiji cha kishoju kata ya kihanga wilayani humo na kusababisha hasara ya shilingi milioni 52.


      Mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Paul Magoryo mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Inspekta Stivedana Webiro amedai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo Februali 5 mwaka huu majira ya saa 9:00 usiku.

    Amewataja watuhumiwa hao mahakamani hapo kwa pamoja kuwa ni Husein Omary,(33) mkazi wa kijiji cha katoro, Abdukarim Kabaju (35) mkazi wa kata ya Nshambya,Abdushakir Gervazi (42) mkazi wa mjini Bukoba,Yakub Swaibu(46) mkazi wa Buyekera,na Mdashiru Wilbroad  (30) mkazi wa kata ya kashai.




Washitakiwa wote kwa pamoja wamekana shitaka linalowakabili na wamerudishwa rumande hadi juni 2 mwaka huu kesi yao itakaposikilizwa tena.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top