Wakristu
wametakiwa kuwa na hamu ya kumpokea bwana Yesu Kristu katika kumtumikia na
kugawana muda wake pamoja naye.
Wito huo
umetolewa leo na Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga Askofu Almachius Vicent Rweyongeza katika
Ibada takatifu ya sherehe ya mwili na damu ya Yesu Kristu yaani Ekaristi
takatifu.
Katika Ibada
hiyo hiyo ya Ekaristi takatifu Askofu Almachius amesema wakiristu wanapaswa kuwa
na hamu ya kumpokea na kugawana muda wao pamoja naye.
Rweyongeza
amesema katika kumpokea Watu wasingangania dhambi hasa kwenye familia ambayo ni
kutopata sekramenti ambayo husababisha ndoa za mitara na kuvunja amri ya sita
ya Mungu na nyinginezo.
Amesema
dhambi hizo ambazo watu wengi huzitenda zimekuwa ni mambo ambayo ni magonjwa ya
kiroho yanayoziba wokovu na uzima wa milele na kusababisha mtu kutoendelea
katika maisha yake.
Askofu
Rweyongeza amesema tiba ya milele katika kufanikiwa ni kujongea sakramenti ya
kitubio ili kuondolewa dhambi na kuweza kupata tija ya kiroho ya Kudumu kwa
kumpokea yesu kristu ambaye ni Ekaristi takatifu.
Katika
sherehe hiyo kumehusishwa misa takatifu, Maandamano ambayo ni kumshudia kiristu
bila aibu kutoka kwa watu kwani anakuwa kwani anayefanya hivyo anakuwa amekiri
adharani mbele ya watu wengine kwamba
yeye anamtumikia yesu kristu.
Rweyongeza
amesema njia ya maandamano imepambwa na nyimbo za sifa za kusifu Ekaristi na
maua ambayo ni mwaliko kwa kila mmoja kumpamba yesu kwa kupamba njia ambayo
anapita kwa kutumia upendo, utii, uaminifu, mienendo mizuri ambayo itamfanya
mkiristu naye kuvutia katika maisha yake.
Post a Comment