Wanawake mkoani Mbeya
wametakiwa kujishughulisha katika kubuni mirdi mbalimbali itakayowaisadia
kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili
katika jamii.
Wito huo umetolewa na
kiongozi wa shirika lisilo la kiserikali wilayani Rungwe liitwalo MWEPEA,
mwenyekiti wa asasi hiyo Syoni Malakasuka, amesema kuwa mwanamke ni vema
akawa mbunifu katika kutafuta namna ya kuweza kujikwamua kiuchumi ili
kuondokana na dhana ya kuwategemea waume zao katika mahitaji mbalimbali ya
nyumbani.
Aidha ameongeza kuwa
mwanamke anauwezo mkubwa wa kufanya kazi licha ya wanawake wengine kujiona kama
hawawezi kufanya kazi kama mwanaume, ambapo amesema kuwa hali hiyo inawafanya
waweze kuitwa magolikipa wa nyumba kutokana na uvivu wanaounyesha,hivyo
amewataka wanawake kuweza kujituma katika kazi mbalimbali zinazoweza kuwakomboa
ukiuchumi na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.
Hata hivyo Malakasuka
amesema kuwa shirika hilo limeweza kutoa misaada mbalimbali katika jamii kama
kujenga Mabweni ya wanafunzi wa kike katika Shule za Sekondari pamoja na kutoa
elimu ya jinsia ili kuweza kuepuka mimba zisizotarjiwa hali inayopelekea
kukatishwa masomo na kushusha kiwango cha elimu nchini
Sambamba na hayo
ameiomba Serikali kuweza kuwapa kipaumbele wanawake katika Nyanja
mbalimbali za ajira pamoja na kuwapatia fursa ya kuweza kupata Mikopo kwa
urahisi ili kunusuru hali ya umasikini nchini.
Post a Comment